Ndege aina ya RX1E-A inayotumia umeme iliyoundwa na Chuo Kikuu cha masuala ya anga cha Shenyang imeruka kutoka uwanja wa ndege wa Caihu huko mkoani Shenyang mji mkuu wa Liaoning kaskazini mashariki mwa China.
Kwa mujibu wa makamu wa rais wa Liaoning General Aviation Academy, Zou Haining ni kwamba uboreshaji wa ndege hiyo ni hatua ya kuingia katika masoko ya Marekani na Ulaya. Ndege hiyo ambayo ina uwezo wa mwendo wa kilomita 160 kwa saa, itaweza kutumika kwa ajili ya mafunzo ya urubani, usafiri, utalii na kupiga picha za anga.


Utengenezaji wa kizazi cha kwanza, RX1E, ulianza mapema mwaka 2016 ambapo inabeba abiria wawili kwa sasa inatarajiwa kuendelea kuboreshwa na kuongezwa ukubwa ili iweze kubeba watu wengi zaidi. Ndege hiyo iliruka kipindi cha kati ya dakika 45 hadi saa mbili katika majaribio yake.
