fbpx
simu, Teknolojia

GM 9 Pro simu mpya kutoka Uturuki

gm-9-pro-simu-mpya-kutoka-uturuki
Sambaza

Kampuni ya kisasa ya simu ya kituruki ya General Mobile imezindua simu yake mpya inayofahamika kwa jina la GM9 Pro ambayo ina sifa za kuwa miongoni mwa simu bora duniani.

Miongoni mwa nguvu na ubora wa GM 9 Pro ni kamera nzuri, ujazo mzuri wa betri yake kwa kukaa na chaji kwa muda mrefu pamoja na kuwa na mfumo endeshi wa Android oreo.

INAYOHUSIANA  Tecno M3 na Tecno P3 : Fahamu Tofauti Zake!

Aidha kwa upande wa sauti ipo vizuri pia kulingana na sauti ya simu za Google Pixel 2. Na kwa upande wa kamera ina uwezo wa kurekodi video za 4K.

Wasifu wa GM 9 Pro

 • Mawasiliano: 4G
 • Kioo: AMOLED Full HD, ukubwa wa inchi 6.01Uwezo wa GPU: Adreno 512
 • Uwezo wa Prosesa: Vipuri nane (8)ndani ya moja na kasi 2.2 ya GHz
 • Aina ya Prosesa: Qualcomm Snapdragon 660
 • Mfumo endeshi: Android 8.1 Oreo
 • Ukubwa wa ndani: 64 unaweza kuweka MicroSD mpaka ukubwa wa 256GB
 • Ukubwa wa RAM: 4GB
 • Kamera : Ya nyuma: zipo mbili 12MP + 8 MP na ile ya  mbele ina 8 MP, f / 2.0
 • Ukubwa wa Betri: 3800mAh
 • Ulinzi: Ina uwezo wa kutumia alama ya kidole
 • Redio: FM Radio
 • Bei: 385 USD (Tsh. 870,000/-)
 • Rangi: Fedha, Kahawia na Dhahabu.
Kampuni iliyotengenza GM 9 Pro  kwa sasa simu zao zinauzwa katika mataifa 33 duniani.

Kampuni husika inatarajia kupanua soko lao mpaka kufikia mataifa 45 kabla ya kumalizika mwaka huu wa 2018 na wameweka kiasi cha pesa za kituruki zipatazo milioni 100 za Lira (sawa Tsh. milioni 36,200,000).

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share
Tags: ,

Siyan

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.