Wale wanaojua kufanya mengi kwenye WhatsApp si haba wameshawahi kuweka mpangilio wa kutaka kile ambacho wanakituma kwenda kwa mtu fulani basi kitoweke/kifutike baada ya siku kadhaa kupita. Kuna uwezekano wa kusoma jume zilizotoweka!.
Mara kwa mara WhatsApp imekuwa inafanyiwa maboresho na kabla ya kuruhusu massisho hayo kuwafikia watu wote basi huanzia kwa wale ambao wanatumia toleo la Beta. Fahamu ya kuwa waundaji wa WhatsApp wapo kazini kuleta maboresho ambayo yatawezesha watumiaji kuweza kusoma tena zilie jume ambazo zimetoteka.
Inakuaje hii?
Wengi wetu tunafahamu kipengele cha “Disappearing messages” kwenye WhatsApp kipengele ambacho iwapo mtumiaji atakiruhusu basi jumbe zote ambazo zitafuata baada ya kitufe hicho kuwashwa zitatoweka baada ya siku saba kupita. Sasa katika maboresho ambayo WhatsApp inayafanyia kazi ni uwezekano wa kuweza kusoma kwa mara nyingine tena kile ambacho aliyekituma alilenga kifutike mara baada ya siku saba kupita.

Katika hatua nyingine WhatsApp Desktop ipo mbioni kuboreshwa kwa kumwezesha mtumiaji kuweka maelezo fualni pale anapotaka kumtumia mtu nyaraka kutoka kwenye kompyuta sawa na vile ambavyo inawezekana kuweka maelezo chini ya picha kabla ya kutuma kwenda kwa yule unayetaka kumtumia picha.
Vitu hivi kwa sasa yapo katika hatua ya kutengenezwa na bado haijafahamika ni lini mathalani maboresho ya kuweza kusoma jumbe zilizotoweka yataanza kupatikana lakini kama unataka kuwa miongoni mwa watu ambao wanapata masasisho kabla ya wengine hakikisha unatumia toleo la karibuni kabisa la WhatsApp Beta.
Chanzo: WaBetaInfo
No Comment! Be the first one.