fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

simu Teknolojia Uchambuzi

Uchambuzi kuhusu Xiaomi Redmi Note 8

Uchambuzi kuhusu Xiaomi Redmi Note 8

Spread the love

Xiaomi ni kampuni ya kiteknolojia yenye makao makuu yake nchini Uchina. Inajihusisha na vitu vingi kama Simu za mkononi, vifaa vya nyumbani kama runinga, huduma za uhifadhi wa kimtandao na kadhalika.

Katika nyanja ya simu za mkononi, kampuni ya Xiaomi imejikita katika mlengo mmoja kwa maana ya kwamba kutoa simu zenye ubora mzuri kwa bei rafiki kwa wateja na watumiaji kwa simu kwa ujumla.

Redmi Note 8

Xiaomi Redmi Note 8 inayopatikana kati ya $175~$200 ambazo ni sawa na zaidi ya Tsh. 402,500~Tsh. 460,000.

).

Simu hii ya Redmi Note 8 ni mojawapo katika matoleo yao, yenye ubora wa hali ya juu na thamani nzuri kwa pesa ya mnunuaji. Imejazwa sifa na vifaa mbalimbali kwa gharama rafiki.

Sifa za simu hii ni kama ifuatavyo:-

  • Kioo (Display) cha teknolojia ya LCD cenye ukubwa wa inch 6.3,
  • Mfumo endeshi (OS) wa Android 9.0 (Unaweza kupandishwa hadi Android 10),
  • Kipuri mama ni Qualcomm Snapdragon 665,
  • RAM ya GB 3, 4 ama 6 na diski uhifadhi ya ukubwa wa GB 32, 64 au 128,
  • Mfumo wa kamera nne nyuma (MP 48, 8, 2 na 2) pamoja na kamera ya MP 13 mbele,
  • Betri yenye uwezo wa 4000mAh.
SOMA PIA  Simu ya Rais Donald Trump ina App moja tu!

Simu hii pia inasapoti Teknolojia ya mawasiliano ya 4G, kwa intaneti yenye kasi, pia inasapoti teknolojia ya Bluetooth na WiFi kwa kusirikisha mafile na huduma ya mtandao, sehemu ya kuweka memori ya ziada. Simu hii pia ina huduma ya reddio hivyo kuweza kusikiliza muda wowote.

SOMA PIA  Bibi wa miaka 81 atengeneza app yake ya kwanza kwa ajili ya iOS

Simu hii ina sehemu ya kuchomeka waya wa chaji, aina ya USB Type-C. Pia ina sehemu ya kuchomeka spika za masikioni. Ipo katika matoleo makuu manne ya rangi; Bluu, Nyeupe, Nyeusi na Zambarau.

Vyanzo: GSMArena, Gadgets360.

Joshua Maige

Mkazi wa Dar es Salaam, Tanzania.
Kwa sasa, ni mwanafunzi katika Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam(DIT), pia ni mwandishi wa makala za kiteknolojia katika ukurasa wa Teknokona.

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania