fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

simu Teknolojia Uchambuzi

Uchambuzi wa Samsung Galaxy A21s

Uchambuzi wa Samsung Galaxy A21s

Spread the love

Simu ya Samsung Galaxy A21s ni mojawapo ya matoleo ya chini ya kampuni ya Samsung.

Simu hii ina muundo mzuri na mfumo rahisi kueleweka na kutumika kwa mtu yeyote. Baadhi ya sifa za simu hii ni:

  • Kioo (Display) cha teknolojia ya LCD chenye ukubwa wa inch 6.5,
  • Mfumo Endeshi (OS) wa Android 10,
  • Kipuri mama ni Samsung Exynos 850,
  • RAM ya GB 2,3 au 4 na Diski Uhifadhi yenye ukubwa wa GB 32, 64 au 128,
  • Mfumo wa Camera nne nyuma (MP 48,8,2 na 2) na kamera ya MP 13 mbele,
  • Betri yenye uwezo wa 5000mAh.
SOMA PIA  Taarifa: 80% ya bidhaa za Apple zinatumia iOS 12

Simu hii inakuja na teknolojia ya utambuzi wa alama za vidole. Pia inasapoti teknolojia ya mawasiliano ya 4G kwa mtandao wenye kasi kubwa. Pia, ina huduma za WiFi na Bluetooth kwa jaili ya kushirikisha data na taarifa nyingine. Simu hii pia ina huduma ya FM Radio.

Gslaxy A21s

Samsung Galaxy A21s katika muonekano wa rangi mbalimbali.

.

Simu hii inapatikana kwa angalau shilingi laki nne pesa ya Tanzania, ina sehemu ya kuchomeka waya wa chaji aina ya USB Type-C. Pia ina sehemu ya kuchomeka spika za masikioni. Matoleo ya rangi kwa simu hii ni manne: Nyeupe, Nyeusi, Bluu na Nyekundu.

Je, una maoni gani kuhusu simu janja ambayo imeletwa mbele ya macho siku ya leo? Tungependa kusikia kutoka kwako na daima usiache kutufuatilia kupitia mitandao yetu mbalimbali ya kijamii.

Vyanzo: GSMArena, Gadgets 360.

Joshua Maige

Mkazi wa Dar es Salaam, Tanzania.
Kwa sasa, ni mwanafunzi katika Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam(DIT), pia ni mwandishi wa makala za kiteknolojia katika ukurasa wa Teknokona.

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania