fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Android Review simu Teknolojia

Ifahamu Tecno Phantom Z Mini (V7), Uwezo wa Juu kwa Bei ya Kawaida

Ifahamu Tecno Phantom Z Mini (V7), Uwezo wa Juu kwa Bei ya Kawaida

Spread the love

Siku chache zilizopita nilifanikiwa kuwa karibu na simu janja ya Tecno Phantom Z Mini na ninaweza kusema imenipa kila sababu ya kujipanga ili nami niimiliki. Simu hii imeingia rasmi sokoni mwishoni mwa mwaka 2014.

Phantom Z Mini (V7) imetolewa baada ya mafanikio makubwa ya toleo la Phantom Z liloingia sokoni mwanzoni mwa mwaka jana. Phantom Z Mini ni simu ninayoweza sema ina kila sifa za simu janja (smartphone) bora zaidi kwa kiasi cha kuweza kushindana na ata kuzishinda baadhi ya matoleo ya bei ghari zaidi kutoka kwa makumpuni mengine makubwa ya simu duniani kama Samsung na iPhones. Kumbuka simu za Tecno zinauzwa na kutengenezwa kwa bara la Afrika tuu hivyo ukuaji wake wa kiuwezo katika kuleta simu zenye uwezo wa hali ya juu hivi ni za kufurahia kabisa.

phantom-Z-mini-muonekano-mpya

Nikurudishe mwanzo, niliweza kutumia na kuijaribu simu ya Phatom Z Mini kwa masaa kadhaa na hivi ni baadhi ya vitu nilivyogundua kwa haraka haraka

  • Inakioo (display) chenye uwezo mzuri sana. Muonekano wa picha unamvuto wa kipekee
  • Ina moja ya kamera nzuri zaidi katika soko kwa sasa. Kama wewe ni mpenzi wa kupiga picha, basi Phatom Z Mini inakupa kila sababu ya kuzipenda zaidi picha uzipigazo.
  • Na kwenye suala la kamera, inakamera mbili kama kawaida kwa simu nyingi siku hizi lakini cha kipekee zaidi ni kuwa hadi kamira yake ya mbele kwa ajili ya selfies ina ‘flashi’ pia…yaaani unaweza piga selfies ata kama uko kwenye giza nene!
  • Na ingawa ina uwezo mkubwa sana simu hii  ni nyepesi sana mkononi ukilinganisha na uwezo wake kiutendaji. Ni nyembamba ila yenye mvuto na inakaa vizuri sana kiganjani.
SOMA PIA  Rudisha mafaili yaliyojificha kwenye memori kadi yako!

Baada ya kugundua haya machache nikaamua ni vizuri niichunguze zaidi na kuweza kuwafahamisha kwani kama unafikiria kuvuta simu mpya mwaka huu basi hii ni moja ya simu ya kuiweka kwenye orodha ya chaguo zako.

Sifa Zake kwa Undani;

>Android 4.4

Inatumia programu uendeshaji ya kisasa kabisa ya Android 4.4. Timu ya Tecno wameweza kuiboresha kimuonekano kuipa muonekano unaovutia sana, hawajajaza apps zisizokuwa na ulazima na nzito kama makumpuni mengine yafanyavyo.

>Diski Uhifadhi (Memory Disk), Inakuja na uhifadhi wa GB 16 ambao ni mkubwa wa kutosha kuweka vitu vingi sana . Tumegundua haina sehemu ya kuweka kadi ya ziadi (memory card) lakini kwa ukubwa wa GB 16 unatosha kwa mambo mengi zaidi, na ata kama unataka kuhamisha mafaili basi utumiaji wa waya wa USB -Mini utatusha kabisa.

>Inakioo cha Inchi 5 na kwa kiasi chote sehemu yote ya mbele ya simu hii imechukuliwa na kioo (display) yake.  Na kioo hichi ni cha HD (720*1280) kinachotumia teknolojia maarufu ya Super AMOLED. Kwa kuitumia kwa masaa machache naweza kukubali inaonesha picha na video katika ubora mzuri.

>Laini Mbili – Wengi wetu tunamiliki laini zaidi ya moja ya simu, simu hii inasehemu mbili za kuweka laini. Sehemu moja ni kwa ajili ya laini za ukubwa mkubwa (tuliouzoea wa kadi za laini), wakati mwingine ni wa zile kadi za laini zinazotumika sana kwenye simu za kisasa siku hizi, ukubwa wa Micro (laini ndogo).

SOMA PIA  Mazungumzo ya WhatsApp: Hamisha kutoka Android kwenda iOS

>Je unapenda kupiga selfie?  Kamera yake ya mbele yenye sifa ya uwezo wa kutoa mwangaza (flash) pale picha inapopigwa ina MegaPixels 8 wakati ya nyuma yenye flash pia ina MegaPixels 13. Ukilinganisha kwa haraka, kamera ya nyuma kwenye simu ya Samsung Galaxy S4 nayo ni MegaPixels 13 ila kamera ya mbele (kwa ajili ya selfies 🙂 ) ni MegaPixels 2 tuu!!!!! Hii ni tofauti kubwa sana, na inanifanya kusema kwa mtu yeyote anayependa kamera yenye picha nzuri zaidi basi Tecno Phatom Z Mini inakupa kila sababu ya kuinunua. Pia muonekano wa picha ni wa uzuri wa hali juu.

Mlinganisho wa haraka wa picha zilizopigwa eneo moja na mwanga wa kawaida bila kutumia flash kati ya Galaxy S4 Active na Tecno Phantom Z Mini

Mlinganisho wa haraka wa picha zilizopigwa eneo moja na mwanga wa kawaida bila kutumia flash kati ya Galaxy S4 Active na Tecno Phantom Z Mini

Ubora wa picha za Selfi (kamera ya mbele) ukilinganishwa na Samsung Galaxy S4 Active (MegaPixels 2) na Galaxy S II (MegaPixels  2)

Ubora wa picha za Selfi (kamera ya mbele) ukilinganishwa na Samsung Galaxy S4 Active (MegaPixels 2) na Galaxy S II (MegaPixels 2)

>Betri inayokuja nayo ni yenye kiwango cha kuridhisha, nacho ni cha 2420mAh. Kwa simu janja yenye mambo mengi kiasi ukubwa huu unatosha, (nami naamini hakuna siku zote chaji huwa haitoshi 🙂  )

>RADIO!!!! Ndiyo, tunafahamu sana hiki ni kitu kinachokosekana katika simu janja nyingi siku hizi. Tecno Phantom Z Mini inakuja na app ya radio za FM hivyo kwa wale wanaopenda programu zao spesheli kutoka stensheni za redio ila pia wanapenda simu janja iliyojisholeza kimuonekano basi hiki ni kitu cha kitofauti sana. Siku hizi app ya radio za FM nyingi kwenye simu janja ni zile zinazotumia intaneti, hii utaweza kusikiliza radio bila intaneti. Redio yeyote inayopatikana kitaa utaweza kuisikiliza bila shida.

SOMA PIA  Bana Matumizi ya Intaneti kwenye Simu Yako na Hizi Mbinu

Teknolojia zingine za kimawasiliano zilizopo ni pamoja na GPS (Kwa ajili ya kutambua mahali ulipo), WiFI (Intaneti), Bluetooth, pia waya mdogo wa USB (Kwa ajili ya kuchaji na kuhamisha data). 

Je nini sikukipenda kuhusu Tecno Phantom Z Mini?

Kutokuwepo kwa uwezo wa kuweka kadi ya zaidi ya uhifadhi (memory card/Micro ssd). Kwa wengine linaweza kuwa ni jambo dogo ila kwa baadhi inaweza ikawa ni jambo kubwa. Ila bado uwezo wa kuweza kuhamisha mafaili kupitia USB na pia huduma maarufu za CLOUD kama DropBox kunaondoa kabisa umuhimu wa uwepo wa ‘memory card’ (Bofya HAPA kufahamu kuhusu DropBox).

Je kama unafikiria kununua simu janja (smartphone) tutakushauri ununue hii?

Kwa kiasi kikubwa tunaweza kusema kutokana na sifa zilizonazo ukilanganisha na bei inayouzika Phantom Z Mini ndiyo amuzi sahihi kama unafikiria kununua simu kwa sasa. Bei yake kwa utafiti wa haraka tulioufanya ni kwenye takribani Tsh 470,000/=*, kwa bei hii simu inakuwa ni moja ya simu inayoweza kupewa sifa ya kuuzwa kwa bei ya kawaida sana ukilinganisha na sifa na uwezo wa kiutendaji na muonekano iliyonayo.

Je ushawahi kutumia au bado unatumia simu hii? Tuambie wewe unaionaje? Kumbuka unaweza kutuuliza na kuomba tukuelezee kuhusu simu yeyote uipendayo kupitia barua pepe teknokonatz (at) gmail dot com au kupitia akaunti zetu za Twitter, Facebook na Instagram .

Endelea kusoma TeknoKona!

*MABADILIKO: Kwa taarifa tulizozipata kwenye ukurasa wa Facebook wa Tecno Tanzania simu hii inapatikana kwa Tsh 430,000/= kwenye maduka ya Tecno Tanzania yote.

Comrade Mokiwa

Mbunifu na mpenda teknolojia.

Muanzilishi wa Teknokona, TechMsaada na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Comments

  1. Hamim Sheikhal - July 3, 2015 at 09:15 - Reply

    Habari yako mkuu…. kiukweli mko vizuri hasa katika kutupatia elimu nzuri ya kiteknolojia nimependa sana!!!! Tatizo langu Mimi nilikuwa nstumia simu ya Techno F6 lakini cha kushangaza sasa ivi inaniandikia ” Please Enter The Privacy Protection Password” nimeshindwa kuelewa nisaidieni

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania