Moja ya mtandao mkubwa zaidi wa kijamiii wa Twitter wenye watumiaji zaidi ya milioni 284 kwa siku umeleta vitu vipya zaidi katika huduma yake. Twitter imejikuta ikiitaji kuleta mambo mapya zaidi kwa nia ya kuongeza wastani wa muda watu wanatumia kwenye mtandao huo juu ya upinzani mkali wanaopata kutoka kwenye mitandao mingine ya kijamii iliyoanza hivi karibuni kama vile Instagram.
Sasa wanawawezesha watumiaji wa mtandao huo kuanzisha mazungumzo na watu wengi zaidi kupitia eneo la ujumbe (inbox). Ila utaweza kuanzisha mazungumzo na watu ambao tayari wanakufuatilia (FOLLOW), na si lazima wewe uwe unawa’follow. Mazungumzo haya yaweza kutunzwa (saved) kama kundi (group chats)na hivyo washiriki wanaweza kulipa kundi jina na kuendelea kuchati mara kwa mara.
Kitu kingine ni uwezo wa mtumiaji wa mtandao huo kurekodi na kutuma video fupi za hadi sekunde 30. Tayari mtandao wa Twitter unamiliki Vine, huduma ya kwanza kabisa ambayo kwa kiasi kikubwa inafanana na Instagram, ila ilianza kabla ya Instagram. Kabla ilikuwa inakuitaji pale unapotaka kuweka video kwenye mtandao huo wa Twitter ilibidi iwe ipo kwenye mtandao mwingine kama vile Youtube na Vine, ila sasa utaweza kurekodi na kuweka (upload) video moja kwa moja kwenye Twitter.
Je wewe ni mtumiaji wa Twitter? Umefurahishwa na mabadiliko haya? Unaweza kutuambia kupitia akaunti zetu za Twitter, Facebook na Instagram .
Soma pia;
–Mambo 20 Kuhusu Mtandao Wa Kijamii Wa Twitter!
–Instagram yaipita Twitter Kwa Ukubwa: Mabadiliko Yanakuja!
No Comment! Be the first one.