fbpx

Chimbuko la sarafu ya kidijitali-Diligence

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Katika moja ya vitu ambavyo teknolojia inayokuwa na kuendelea kuvutia na soko la ushindani basi sarafu za kidijiti zipo na zinaendelea kubuniwa kila leo, Tanzania zipo kadhaa na mojawapo ni Diligence.

Moja ya sababu ya mambo kwenda sawia/kama ilivyotarajiwa ni baada ya kufanyika utafiti wa kina kabla ya kuanza kutumika na ni hivyo hivyo kwa sarafu ya kidijiti, Diligence.

iRA ni nini?

iRA (incentive Research Africa) ni mpango ambao unahusisha masuala ya utafiti. Utafiti huo unafanyika kwa njia ya mtandao (online) ukihusisha mambo ya kiuchumi, kisiasa, kijamii, kiteknolojia barani Afrika.

Deligence ni nini?

Diligence ni sarafu ya kidijitali ambayo itakuwa ikiupa nguvu mfumo wa iRA kama njia ya malipo. Imetengenezwa katika mfumo wa Ethereum. Kuna sarafu za Diligence mil 21 tuu.

diligence

Nembo ya sarafu ya kidijiti-Diligence.

Kwa nini iRA?

👉Kutambua umuhimu wa mtu anayefanyiwa utafiti na kuufanya utafiti kama moja ya kazi zinazoingiza kipato.

INAYOHUSIANA  Microsoft Walitumia Nini Kuwafunza Watu Kutumia Kipanya?

👉Watu wengi watashiriki utafiti ndani ya mda mfupi na kupata matokeo sahihi

👉Itazuia upikaji wa taarifa za tafiti.

👉Mtu atakayeshiriki hizo tafiti atalipwa kwa sarafu ya kidijitali ijulikanayo kwa jina la Diligence.

iRA itafanyaje kazi?

iRA itamtambua kila mtumiaji kwa kumjua kila mteja wake ambapo kutokana na kuwa na kanzi data ya iRA. Taarifa za mtumiaji zitahifadhiwa salama ili kusaidia tafiti zinazokuja ziwafikie walengwa.

Kila tafiti inayokuja itawafikia wahusika tu.

🎈Mtu ataletewa maswali na atayajibu mtandaoni na baada tu ya kuyajibu atatuma na ajili ya uhakiki.

🎈Mtu akishamaliza kujibu maswali atalipwa sarafu ya Diligence Maana ndani ya iRA kutakuwa na mfuko wa kidijitali wenye uwezo wa kuitunza sarafu ya iRA. Hivyo, baada tu ya kazi ya kujibu maswali mtu atalipwa.

Hatua iliyopo iRA kwa sasa.

Kuuza asilimia 40 ya sarafu za Diligence duniani kote ili kupata hela ya kuendesha mipango yake ambapo mauzo ya sarafu Diligence yameanza Desemba, Mosi 2018 hadi Februari, 28 2019.

diligence

Mpango kazi wa iRA/Sarafu ya kidijiti-Diligence.

Kwa maelezo zaidi unaweza kutembelea iradiligence.com kuweza kufahamu mengi kuhusu iRA na sarafu ya Diligence kwa ujumla.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.