Snapchat imeendelea kuwakosha watumiaji wake kwa kuzidi kuwaletea mambo mapya na yakuwafurahisha kila siku, leo mtandao huo umeingia katika vichwa vya habari vya mitandao mingi baada ya kuanzisha emoji zinazotembea katika video.
Snapchat imetoa toleo jipya kwa watumiaji wa Android ambalo pamoja na mambo mengine limeleta emoji zinazotembea na video, emoji hizi zinaweza kuwekwa katika vitu ambavyo vinatembea katika video na hivyo emoji ikawa inatembea na kitu hicho mfano ni video ya paka ikiwekwa emoji ya uso wa paka kisha paka anavyotembea ile emoji inakuwa inatembea nae.
Kwa ambao hawatapenda emoji za kutembea katika video wanaweza kuendelea na kutumia emoji mgando kama zamani, hii itawafanya watumiaji wote (wasiofurahia na wanaofurahia emoji hizi zinazotembea) kuendelea kuufurahia mtandao huu.
Kwa watumiaji wa iOS wao toleo hili jipya la Snapchat linakuja hivi karibuni, lakini kwa sasa itawabidi kuendelea kushangaa watumiji wa Android wakiji Snapchatisha kivingine.
Mtandao huu ulipoingia ulizaniwa kwamba usingedumu ama usingeweza kuwa na ushawishi mkubwa kwa watumiaji lakini siku zinavyoenda mtandao huu unazidi kuthibisha kwamba umekuja na utakuwepo kwa muda mrefu saana.