fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Mtandao Tovuti

Google Chrome na Mozilla Zimeifungia ‘KickAss Torrents’ Kama Mtandao Wa Udanganyifu!

Google Chrome na Mozilla Zimeifungia ‘KickAss Torrents’ Kama Mtandao Wa Udanganyifu!

Spread the love

Kama ulizoea kupakua mafaili yako tofauti tofauti kutoka katika mtandao huo kupitia katika vivijari vyako vya Google Chrome na Mozila Firefox kwa sasa mbinu zako zitagonga mwamba.

Mtandao huo umefutwa na Mozila pamoja na Chrome kiasi cha kwamba ukijaribu kuingia utapata ujumbe ambao unakwambia huwezi ingia katika mtandao huo.

Kuzuiwa huku ni kwa http://kat.cr na matokeo yote ya Google Search ya https://kat.cr kwa pamoja. Usiku wa jana nilikua na mpango wa kushusha mafaili kadhaa toka katika mtandao huo lakini kila nikiingia ilikuwa inanikatalia. Nipo hapo nilipofanya kautafiti kangu na kunadika makala hii.

Ujumbe Unaoupata Katika Kivinjari Cha Chrome Ukiwa Unajaribu Kuingia Katika Mtandao Huo

Ujumbe Unaoupata Katika Kivinjari Cha Chrome Ukiwa Unajaribu Kuingia Katika Mtandao Huo

Lakini kizuri kuhusu sisi Teknokona huwa tunakuja njia mbadala na tunayofuraha kukuambia kuwa suluhisho tunalo.

SOMA PIA  Tajiri wa Alibaba kujiuzulu nafasi yake

Ili kuweza kuupata mtandao huo tena inakubidi kubadilisha kivinjari, yaani usitumie Chrome wala Firefox. Kwa mfano mimi baada ya hali ile kutokea nilifanikiwa kuingia katika mtandao kwa kutumia Kivinjari cha Edge kutoka Microsoft.

Kingine cha muhimu ni kwamba usiutafute mtandao huo kwa kutumia Google hata kama ukiwa unatumia kivinjari ambacho sio Firefox au Chrome kwani kuna hati hati mtandao huo ukagoma kufunguka pia.

Kwa hili mimi niliingia kwa kupitia kivinjari cha Edge na kisha nikaenda kwenye mtandao maarufu wa utafutaji wa Bing (ambao una nguvu kama google vile). Baada ya kufika hapo nikautafuta mtandao na nikaingi kilaini kabisa. Inavyosemekana muda huu ambao unasoma makala hii naweza nikawa napitia mafaili yangu niliyoyashusha kupita KickAss Torrent (KAT)

Ujumbe Unaoupata Katika Kivinjari Cha Firefox Ukiwa Unajaribu Kuingia Katika Mtandao Huo

Ujumbe Unaoupata Katika Kivinjari Cha Firefox Ukiwa Unajaribu Kuingia Katika Mtandao Huo.

Makampuni yote mawili ambayo yanamiliki vivinjari hivi yamejitetea kuwa yamefanya hivyo kwa makusudi kabisa na lengo lao kuu ni kuhakikisha wanalinda usalama wa watumiaji wao.

SOMA PIA  TikTok Katika Majaribio Ya Kipengele Cha Uzuizi Kwenye Video Zake Za LIVE!

Kumbuka lakini hii sio mara ya kwanza kwa mtandao huu – au kama hii – kupatwa na majanga ya kufungiwa au kutopatikana kwa baadhi ya maeneo au vifaa.

Mitandao hii pia inapigwa vita sana na watu kwani watu wanapata vitu vingi sana kinyemela kwa kutumia hii mitandao. Vitu ambavyo kwa hali ya kawaida ilibidi wavilipie ili wavipate

SOMA PIA  Yahoo! yasogeza mbele mwisho wa kupokea Zabuni

[Maendelea mapya: Tayari team ya KickAss imesema imerekebisha mapungufu ya kiufundi na usalama yaliyosababisha kufungiwa kwao na tayari wanawasiliana na Google na Mozilla ili kuondolewa kwenye orodha ya mitandao isiyo salama. Hili lilishawahi tokea kabla miaka ya nyuma na wakarekebisha na kuachiwa. Inaweza chukua masaa hadi siku kadhaa.]

Niambie kufungiwa kwa mtandao huu kwa vivinjari hivyo viwili wewe jambo hili unalichukuliaje? Niandikie sehemu ya comment hapo chini. Tembelea TeknoKona Kila Siku Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

TeknoKona Teknolojia Tanzania