fbpx
Anga, Roketi, SpaceX, Teknolojia

Mteja wa kwanza kwenda kwenye mwezi na SapceX afahamika

kwenda-kwenye-mwezi-na-spacex
Sambaza

Kama utakuwa ni mfuatiliaji mzuri wa habari za teknolojia utakuwa umeshawahi kusoma kuhusu mpango wa bilionea Elon Musk kupeleka watu kwenye Mwezi kwa kutumia kifaa kilichotengenezwa na kampuni yake.

Wakati fulani Bw. Musk alitangaza kuwa ameshapa mteja wa kwanza atakayefanya safari ya kwenda kwenye Mwezi mwaka 2023 lakini hakumuweka wazi; sasa mwaka huu Sept. 17 jina la mteja huyo amelitaja yeye mwenyewe.

Mtu wa kwanza kwenda kwenye safari hiyo ya binafsi ni Bw. Yusaku Maezawa ambae ni bilionea kutoka Japan, mwanzilishi na Afisa Mkuu Mtendaji wa duka la mtandaoni kuhusu mambo ya urembo, Zozo.

kwenda kwenye mwezi
Bw. Elon Musk akitamtambulisha bilionea Yusaku Maezawa kama mteja wake wa kwanza kwa safari ya kwenda kwenye Mwezi mwaka 2023.

Bw. Yusaku Maezawa ambae anafahamika vyema nje ya Japan kwa rekodi ya kununua picha ya mwaka 1982 iliyochorwa na Michel Basquiat kwa thamani ya $110m. Katika safari yake anaweza akawaalika wasanii 6-8 kuungana nae kwenye safari hiyo.

Mpaka sasa ni wana anga ishirini na wanne (24) tu ndio waliweza kwnda nje ya uzio wa uso wa Dunia safari iliyoanza Desemba 1968-Desemba 1972.

Safari hiyo ya kwanza (kibiashara na kibinafsi) kwa SpaceX inatazamiwa itakuwa ya kihistoria na kuweza kubuni chanzo kipya cha mapato kwa kampuni hiyo.

Vyanzo: Reuters, The Verge

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Karma: Falme za Kiarabu ilidukua simu za iPhones nyingi za wapinzani wake! #Skendo
0 Comments
Share
Tags: , , ,

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|