fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
iOS

Fununu Za Ujio Wa iOS 10: Maboresho Kibao!

Fununu Za Ujio Wa iOS 10: Maboresho Kibao!

Spread the love

Maswali mengi sana watu wanajiuliza ni nini kitakuwa kipya katika programu endeshaji (OS) ya iOS kutoka Apple. Mbali na maswali yahoo lakini kuna taarifa juu ya vitu ambavyo vitakuwepo kwa toleo hilo la iOS.

Jibu kamili naweza nisikupatie lakini nikakupa mwanga juu ya kitu gani kinakuja kwani jibu kamili tutalipata mwezi wa 6 ambapo mkutano mkubwa wa dunia wa ma ‘Developer’ utafanyika.

Kama kawaida yao Apple baada ya mkutano huo tuu huwa wanatoa toleo la kwanza la iOS ambalo linaweza kutumiwa na wataalamu na kuboreshwa (Beta).

Muonekano Wa Kutengeneza Wa iOS 10

Muonekano Wa Kutengeneza Wa iOS 10

Lakini hili sio la kushangaza kabisa kwani kampuni hilo kila linaposemaga linaandaa mkutano basi dunia nzima inakuwa na hamu ya kutaka kujua nini kitatokea.

SOMA PIA  Wasogeze karibu mpaka watu sita unaowasiliana nao kwenye Twitter

Haya Ni Baadhi Ya Mambo Ambayo Yatakuwepo Tuu Katika iOS 10.

• Uwezo Wa Kufuta Au Kuficha App Zinazokuja Na Simu
Hili litakuwa ni jambo jipya na la kihistoria kabisa. Tunajua kuwa makampuni ya simu huwa yanauza simu zikiwa tayari na baadhi ya App ambazo tunaweza kuzitumia. Lakini ukweli ni kwamba App hizo huwa tunazitumia kwa uchache sana au zingine hatuzitumii kabisa. Sasa kama hatuzitumii kwa nini tusizifute? Kumbuka kama kuna App hizi pia zinajaza ujazo wa uhifadhi wa vifaa vyetu.

Lakini tukae mkao wa kula kampuni la Apple linaweza likawa limeleta suluhisho tosha kwa watumiaji wa vifaa vyake. App usiyoipenda unaifutilia mbali au kama ukiona vipi unaificha na inakuwa haionekani. Lakini hapa inawezekana sio kila App ikiwa inaweza kufutwa kwani kuna nyingine ni muhimu sana kama vile App Store na iTunes Store.

SOMA PIA  Clubhouse inaboreshwa kuweza kualika watu wengi

• Maboresho Katika Emoji
Kuingia katika iOS mpya bila matoleo mapya ya Emoji itakuwa ni jambo la ajabu kidogo sio? Ndio! hata kampuni inalitambua hilo kwahiyo limejipanga vikamilifu

Taarifa iliyopo mpaka sasa ni kwamba kampuni la Apple limeshaingia katika makubaliano na kampuni ambalo linatengeneza na lina mamlaka yote kuhusu Emoji, UniCode. Kwa makubaliano ya Unicode na Apple kuna uwezekano mkubwa wa kuwa na Emoji 74 mpya ambazo zitakuja na iOS 10.

• App Nzuri Zaidi Ya Picha
App ya picha kutoka katika kampuni la Apple pia inategemea kufanyiwa manjonjo ya aina yake. Mambo mengi yameongelewa kuhusiana na hili kama vile kuna fununu kuwa mtu anaweza akahariri (edit) eneo Fulani la picha alioipiga katika App hiyo.

SOMA PIA  Kim Kardashian: Hollywood - Gemu linaloingiza BILIONI 1.1 kwa SIKU

Na pia App ya zamani kabla ya hii yaani iPhoto inaweza ikarudi na kupandikizwa ndani ya hii App.

Muonekano Wa iOS 9

Licha Ya Haya Tunagemea Mengi Kuja

Ukiachana na hayo macheche bado tunategemea mambo mengi sana kutoka kwa kampuni ya Apple kwa ujio wa iOS 10. Mkutano unakaribia na ukifikia tutajua mengi zaidi. Sipati picha siku hiyo maana zitajaa habari kutoka Apple tuu kama kawaida yao wakifanya mikutano.

Niandikie sehemu ya comment hapo chini wewe unahisi ni kitu gani kitaongezeka katika iOs 10 kutoka Apple ambacho unahisi mimi sijakisema?. Tembelea TeknoKona kila siku maana ndio GWIJI la habari za kiteknolojia. Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

TeknoKona Teknolojia Tanzania