Changamoto, kupata faida/hasara kwenye biashara ni jambo la ambalo linafahamika na kwa namba inawezekana kuonekana ni ndogo lakini kwa yale waliyoyapitia katika kipindi cha miaka kumi sio kitu kidogo.
Mwezi Julai 2008 ndio soko la programu tumishi lililopo chini ya Apple lilianzishwa na lilikuwa na programu tumishi 500 tuu. Mwazilishi mwenza wa Apple, marehemu Steve Jobs alitabiri Apple Store itakuwa na mafanikio na ndio kitu kinachoonekana kwa sasa.
Katika kipindi cha muongo mmoja App Store imeweza kuwa soko la programu tumishi takribani milioni 2 mpaka hivi sasa.
Katika kipindi cha mwezi ilipoanzishwa iliweza kuwa na programu tumishi 11,500 na kuweza kuwalipa waliozitengeneza takribani $21 milioni.
Mafanikio ya App Store yamechagizwa na nini?
Wakati fulani kwenye mahojiano Steve Jobs aliulizwa kufanikiwa kwa App Store kumetokana na nini? Akaweka wazi sababu/vipengele vikuu viwili tu; mahtaji na mabadiliko ya teknolojia.
Kwanini mahitaji? Katika mwezi mmoja tu takribani milioni 60 waliweza kupakuwa programu tumishi kutoka kwenye App Store. Hivi leo idadi ya wanaopakuwa programu mbalimbali kutoka kwenye soko la programu tumishi lililo chini ya Apple imeongezeka sana.
Programu tumishi zilizoshushwa kwa wingi katika kipindi cha muongo mmoja ndani ya App Store.
Mabadiliko ya teknolojia. Hiki ni kitu ambacho hakopingiki, kutokana na teknolojia kubadilika imekuwa ni chanzo cha mapato kwa wengi na kwa upande wa wanaounda programu tumishi mpaka mwaka 2018 wameweka kupata jumla ya $100bn kutoka $21 milioni miaka 10 iliyopita.
Marehemu Steve Jobs aliona kuwa miechezo (magemu) sio kitu cha kupuuzia hivyo aliwezaalweza kukaribisha magemu kama Nintendo na Sony handhelds ambapo magemu mengine yalikuwa yanapatika bure na mengine ni ya kulipia mpaka hivi leo.
Soko la programu tumishi lililojaa programu kadha wa kadha.
App Store inaendelea kuwa na watu wengi wanaopita kwenye soko hilo kila siku kutokana na mahitaji ya kile ambacho kinaona kinawafaa kwenye simu zao. Miaka inaenda na haionekani dalili za soko hilo la programu tumishi kutetereka.
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.
Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.
Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|