Apple inatarajiwa kuliteka soko mwezi wa tisa ambapo kampuni litaweka sokoni simu zake mpya za iPhone 7 na iPhone 7 Plus. Simu hizi zinategemewa kuwa na maboresho mengi kuanzia ndani mpaka nje.
Ripoti iliyopo ni kwamba matoleo ya simu hizi yatakuwa na mabadiliko ya maumbile ukilinganisha nay ale ya mwanzo. Simu hizi zitakuwa nyembamba na nyepesi zaidi ya yale matoleo ya iPhone 6.
Sawa watumiaji wa iPhone 6s na 6s Plus wanaweza wasiwe na mambo mengi ya kupitwa na matoleo ya simu za iPhone 7 lakini kitu ambacho watapitwa ni uwezo wa Betri.
Katika moja ya vitu ambacho Apple wamejipanga sana katika simu za iPhone 7 ni uwezo wa betri. Simu hizi zitakuja na uwezo wa betri mkubwa ili kuhakikisha simu ya mtumiaji inakaa na chaji muda mrefu
Katika dunia ya simu janja siku hizi tatizo kubwa ni uwezo wa simu hizi kukaa na chaji kwa muda mrefu. Asilimia nyingi ya watumiaji wa simu janja huwa wanatumia mabetri ya nje kuchaji vifaa vya hapa na pale maarufu kama ‘Power Bank’
Betri mpya zitakazokuwa katika iPhone 7 zitakuwa na Wati 7.04 kwa saa. Hili litakuwa ni boresho la aina yake kwani yale matoleo ya iPhone 6s na 6s Plus yana Wati 6.61 kwa saa.
Watu kutoka kiwandani wametoa siri kwa kusema kuwa iPhone za matoleo yanayokuja yatakuwa na mfumo mpya wa CPU (Prosesa). Mfumo huu utakuwa ni ule wa A10 na RAM yake itakuwa ni yenye ujazo wa GB 3 kama sio zaidi ya hapo. Matoleo ya 6S na 6s Plus yana ujazo wa RAM GB 2