fbpx

Samsung Galaxy S10 kuwa na mfuko wa kuhifadhi sarafu za kidijiti

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Mataifa mengi duniani yanaangazia teknolojia/matumizi ya sarafu za kidijitali kama mkombozi wa uchumi wao mbali na hapo hata makampuni ya simu yameona kuna umuhimu wa kuiweka teknolojia hiyo kwenye rununu.

Ikiwa kama mojawapo ya simu ambazo zinazungumzwa sana kuhusiana na sifa ilizonazo leo kwa mara nyingine picha zilizovuja zimeonyesha kuwa Samsung Galaxy S10 itakuwa na mvuto kwa wale wanajihusisha na biashara ya sarafu za kidijiti.

Hii inatokana na picha zilizovuja zikionyesha simu hiyo (Samsung Galaxy S10) kuwa na kipengele cha kuweza kuhifadhi sarafu ya  Ethereum (ETH) pekee huku mtu akiwa na uwezo wa kurudisha mfuko (wallet) wake wa zamani au kutengeneza mpya.

kuhifadhi sarafu

Picha zilizovuja zikionyesha Samsung Galaxy S10 kuwa na kupengele cha kuwa na mfuwa wa kuhifadhi sarafu ya Ethereum (ETH).

Je, Samsung Galaxy S10 itauzwa kiasi gani?

Kama mtu ambae una uza na kununua sarafu za kidijitali unaweza ukavutiwa na simu hii hivyo basi ni muhimu kujiandaa kutenga kiasi cha pesa ili uweze kuinunua:

INAYOHUSIANA  Jinsi Ya Ku Share Mafaili Kati Ya iPhone, iPad na Mac Kupitia AirDrop!

Simu

RAM/Diski uhifadhi/Bei

Samsung Galaxy S10 6GB/128GGB ni $1,210|zaidi ya Tsh.2,783,000
Samsung Galaxy S10+ Lite 6GB/128GB ni $1,015|zaidi ya Tsh. 2,334, 500
Samsung Galaxy S10+ 12GB/1TB ni $2,083|zaidi ya Tsh. 4,790,900

Simu hizo pamoja na nyinginezo kutoka Samsung huenda zitazinduliwa Februari 20 2019. Pamoja na hayo Samsung Galaxy S10 Plus inaelezwa kuwa na teknolojia ya kuweza kupokea chaji kutoka kwa simu nyingine ambayo ina uwezo huo pia (Kiingereza-Wireless reverse charging).

Vyanzo: GSMArena, Ethereum World News

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.