fbpx

Meizu Zero: Simu isiyokuwa na mengi tuliyoyazoea

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Simu janja zinatengenezwa kila leo na hivyo kufanya sisi wanunuzi kuwa na wakati mgumu kutulia na simu moja kwa muda mrefu kwani zinazotoka zinavutia nyingine hazina mengi tuliyoyazoea hivyo kufanya zivutie zaidi.

Teknolojia inakuwa na hivyo basi mambo yanabadilika  kutokana na ubunifu ambao unatuletea kitu kipya bila kusahau ushindani wa kibiashara kutoka kwa wengine wanaofanya biashara hiyo.

Meizu Zero ni simu janja ambayo inaweza ikakushangaza iwapo sio mtu ambae unapenda kujua mambo mapya kwenye teknolojia za kwenye simu na hii ni kwa sababu rununu husika haina yale mengi tuliyoyazoea kuona kwenye simu. Fuatana nami kuweza kujua:

  • Meizu Zero haina kitufe chochote cha kushikika (kitufe cha kuzima/kuwasha, kuongeza au kupunguza sauti havipo)-inatumia teknolojia ya mguso sehemu ileile ambapo huwa vinakuwepo kufanya kazi hiyo.
  • haina sehemu ya kuchomeka USB. Hii ina maana ya kwamba teknolojia ya kuchaji bila na kwa haraka (18W-nguvu ya juu kabisa mpaka hivi sasa) waya ndio inatumika na kama ukitaka kuhamisha kitu kutoka kwenye kmpyuta kwenda kwenye simu au kinyume chake itakubidi utumie Bluetooth tu. Upande wa intaneti ni Wi-Fi au mobile networks pekee.
  • haina sehemu ya kuweka kadi ya simu; inatumia teknolojia ya eSIM.
    mengi tuliyoyazoea

    Inatumia teknolojia ya IP68 kuzuia kuingia maji.

     

Yakiyomo (vitu vilivyopo).

Kipuri mama/KiooSnapdragon 845 ndio uti wa mgongo wa simu husika huku kioo chake kikielezwa kuwa na urefu wa inchi 5.9 ubora wa AMOLED.

Kamera. Kamera zake zimetengenezwa na Sony; upande wa nyuma ina kamera mbili zikiwa na MP 12+MP 20. Kwa mbele ina kamera moja tu yenye MP 20.

mengi tuliyoyazoea

Teknolojia ya alama ya kidole ipo lakini ni ile ambayo imejengewa ndani kes ndani. Rangi Nyeusi/Nyeupe ndio zilizopo kwenye simu husika.

Betri/RAM/Doski uhifadhi na bei. Vyote hivi bado havijaweza kufahamika kutokana na kwamba wahusika hawajaviweka wazi.

Vyanzo: BGR, GSMArena

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Jinsi Ya Kusafisha KeyBoard Ya Kompyuta!
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.