fbpx
Teknolojia

Simu mpya ya BlackBerry, ifahamu BlackBerry KEYone! #2017

simu-mpya-ya-blackberry-ifahamu-blackberry-keyone-2017

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163
Sambaza

BlackBerry KEYone ni simu janja mpya inayovutia itakayoanza kupatikana mwezi wa nne mwaka huu.

Ingawa inatumia jina la BlackBerry utengenezaji mzima umefanywa na kampuni ya TLC ambayo ilinunua hakimiliki ya utengenezaji wa simu zinazotumia jina hilo kwa ushirikiano na kampuni mama ya BlackBerry nchini Kanada.

 Simu mpya ya BlackBerry

BlackBerry Keyone inakuja na keyboard zilizozoeleka katika simu za BlackBerry na pia kioo chake ni cha mguso (touch screen). Simu hii imetambulishwa rasmi katika kongamano la masuala ya kiteknolojia jijini Barcelona nchini Uhispania.

Ingawa utengenezaji unafanywa na kampuni ya TLC bado masuala ya kiteknolojia zinazotumika ndani yake zinatengenezwa na kusimamiwa na BlackBerry, na hii ndio simu yao ya kwanza na kiukweli inavutia.

INAYOHUSIANA  Chagua Simu Nzuri kwa Kuzingatia Haya Machache

Keyboard janja?

 Simu mpya ya BlackBerry

Simu hii inakuja na teknolojia ya kuvutia ambayo BlackBerry walishaanza kuitambulisha, unaweza kutengeneza ‘shortcuts’ za mambo mbalimbali ya kwenye simu hii kwa kutumia Keyboard zake. Mfano unaweza weka mpangilio (setting) ya kufanya app kama Uber kufunguka pale utakapobonyeza na kushikilia herufi U katika keyboard.

Sifa zake:

  • Inakuja na Android Nougat 7.1 ikiwa pia na teknolojia na apps za kiusalama mbalimbali za BlackBerry.
  • Prosesa ya Qualcomm Snapdragon 625 Octa-core ikipewa nguvu na RAM ya GB 3
  • Diski uhifadhi ya GB 32 na uwezo wa kutumia memori kadi (Micro SD)
  • Betri la mAh 3,505, ikiwa na teknolojia ya Quick Charge 3.0 ili kufanikisha chaji kujaa haraka zaidi.
  • Ingawa inakuja na Keyboard pia kioo chake ni cha touchscreen na cha ukubwa wa inchi 4.5 (Resolution Pixel 1620×1080)
  • Kamera ya MP 12 iliyotengenezwa na Sony. Inakuja na uwezo wa video za 4K (30FPS, f/2.0 lense). Kamera ya selfi ni ya MP 8.
  • Pia kwa ajili ya kuchaji inakuja na teknolojia ya kisasa ya USB-C.
INAYOHUSIANA  Ecocapsule: Kijumba Kiduchu cha Umbo la Yai Kwa Ajili ya Makazi ya Kisasa Zaidi

Ingawa BlackBerry wenyewe wamejikita zaidi sasa hivi katika utengenezaji wa teknolojia na huduma za kiusalama zaidi inaonekana jina la biashara yao ya simu imepata mshirika anayejua anachofanya. BlackBerry KEYone ni simu inayovutia na yenye ubora wa hali ya juu.

Bei?

 Simu mpya ya BlackBerry

Kama kuna kitu kinachoweza athiri ufanyaji mzuri sokoni wa simu hii basi ni bei yake. Simu hii inayotegemewa kuanza kupatikana mwezi wa nne mwaka huu itauzwa kwa Dola 549 za Kimarekani, hii ni takribani Tsh 1,227,000/=. Hii ni pesa nyingi sana na suala la bei ndilo lilokuwa kikwazo kwa matoleo mengine kadhaa ya Android ambayo BlackBerry wenyewe walitoa katika kipindi cha miezi 24 iliyopita.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |