fbpx

Uchina: App kukutaarifu watu wenye madeni ya mikopo benki wakiwa karibu yako

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Mahakama ya mkoa fulani nchini Uchina imekuja na teknolojia inayokupa taarifa kama kuna watu karibu yako wenye madeni benki. App ya kukutaarifu watu wenye madeni ya mikopo benki wakiwa karibu yako ni moja ya app ambazo usingeweza kufikiri zinaitajika.

wechat App kukutaarifu watu wenye madeni

App kukutaarifu watu wenye madeni: Teknolojia hiyo inatumia app maarufu nchini Uchina, WeChat

Mfumo huu umeletwa kama kuongoza msokumo wa kijamii kwa wenye madeni benki kuweza kuanza kulipa madeni yao. Mfumo huo umeingizwa kwenye app maarufu ya WeChat.

INAYOHUSIANA  Twitter kuongeza idadi ya maneno ya kuandika ujumbe

Uwezo ndani ya app hiyo?

App kukutaarifu watu wenye madeni

Laolai Map: Muonekano wa ramani ya ndani ya app ya WeChat. App ikionyesha watu mbalimbali na taarifa zao kama vile majina na kukwambia kuhusu madeni yao

> Watu wenye madeni wakiwa karibu yako angalau ndani ya mita 500 utapata kuwaona kwenye ramani ya ndani ya app ya WeChat.

> Pia mtu anayetumia app hiyo anaweza kutoa taarifa juu ya watu anaodhani wana uwezo wa kulipa madeni yao. Hii inaweza ikawa kwa jinsi anavyoona wanavyoishi.

INAYOHUSIANA  Facebook kuja na Mfumo wa Magemu - kama vile Steam

Serikali ya Uchina inafanya jitihada kubwa ya kuhakikisha watu wenye madeni wanalipa kwa wakati. Tayari kuna utaratibu umewekwa ambapo watu wenye madeni ambayo hayalipwi kisahihi au kwa wakati hawana ruhusa za kusafiri kiutalii nje ya nchi au kupeleka watoto wao kwenye shule za ada za juu.

Ramani hiyo ndani ya WeChat imepewa jina la Laolai Map, neno “Laolai” ni neno la dharau linalotumiwa kwa watu ambao wanaoshindwa kulipa madeni yao ya pesa nchini humo.

INAYOHUSIANA  Nunua Bidhaa Instagram: Instagram wanakuja na huduma ya manunuzi

App hiyo itagundua watu ambao hata si marafiki wa wengine kwenye WeChat na kisha itampa uwezo mtumiaji app kusambaza wasifu (profile) wa mtu huyo kwenye chapisho (status) au kuweza kuripoti kwa mahakama.

Vipi una mtazamo gani juu ya app hii?

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.