fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Sarafu za kidijitali Teknolojia

Japan kufanya utafiti zaidi kuhusu sarafu za kidijitali

Spread the love

Kwenye ulimwengu wa sasa matumizi ya sarafu za kidijitali yameendelea kushika kasi igawa serikali za nchi nyingi bado hazijahalalisha matumizi rasmi hasa kwenye mabenki na serikali ya Japan bado inaona inahitaji kuweka nguvu zaidi kwenye utafiti kuhusu sarafu hizo ambazo hazishikiki.

Sarafu za kidijiti zipo nyingi kwa idadi mfano Libra, Diligence, XRP, Bitcoin Cash, Ethereum, Litecoin, n.k lakini inayoongoza kwa thamani ni Bitcoin (BTC). Kwa miaka kadhaa sasa mtu anaweza kufanya malipo ya kitu fulani kwa kutumia sarafu za kidijitali mathalani kwenye migahawa, kununua tiketi ya ndege.

SOMA PIA  Uwezo wa kuzuia makelele kwenye Zoom Meeting

Japan nchi mojawapo ambayo watu wanaweza kuliupia huduma mbalimbali kwa kutumia sarafu za kidijitali lakini kwa mujibu wa taarifa ya karibuni nchi hiyo imeamua kuwekeza zaidi kwenye kufanya utafiti zaidi kabla ya kuweza kuwekwa kwenye mzunguko wa mabenki. Serikali ya nchi hiyo imeweka wazi kuwa haina mpango wa karibuni kufanya sarafu hizo zitumike benki kuu lakini ni kitu ambacho wanakitilia maanani. HIvyo, wizara zinazohusika zitafanya utafiti wa kina kisha kuja na sababu kwanini sarafu hizo zitumike bila kusahau faidda/hasara zake kwenye mfumo wa fedha.

utafiti

India, Pakistan, Colombia, Canada, na Nigeria ndio nchi ambazo zinatajwa kufanya miamala ya sarafu za kidijitali. Ugiriki na Romania ndio nchi ambazo wanawake wengi wamejitosa kwenye ulingo huo.

Daima Japan imekuwa mwangalifu sana kuhusu kukimbilia ukuaji wa sarafu za kidijiti kwa sababu ya kuhofia kutikisa mzunguko wa fedha kutokana na kwamba wananchi wake wanapenda kutumia pesa zinazoshikika.

Vyanzo: Gadgets 360, Japan Times

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania