fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
apps Mtandao Mtandao wa Kijamii Teknolojia TikTok

Pengine App Ya Usambazaji Wa Muziki (Kama Spotify) Kutoka TikTok Iko Njiani!

Pengine App Ya Usambazaji Wa Muziki (Kama Spotify) Kutoka TikTok Iko Njiani!

Spread the love

Ni wazi TikTok ni moja kati ya mtandao ya kijamii ambao inapata ukuaji mkubwa sana kwa kipindi cha muda mfupi

Licha ya mafanikio hayo bado mtandao wa TikTok unajulikana kama njia kubwa sana inayotumika na watu katika kugundua vipaji

TikTokVipaji hivyo ni kadha wa kadha ikiwemo na ugunduzi wa vipaji vya mziki. Kupitia mtandao huo wa TikTok vipaji vingi sana vimegunduliwa

Mitandao ya kijamii huwa na kawaida kuwa na nguvu kubwa sana katika ugunduzi wa vipaji. Unakumbuka Justin Bieber alivyogunduliwa na meneja wake kupitia mtandao wa kijamii wa Youtube? Fikiri ukubwa wa Justin Bieber sasa?

SOMA PIA  Acer kuingia kwenye biashara ya runinga janja

Turudi TikTok, kampuni ambayo inamiliki mtandao huu (ByteDance) ni kampuni ambayo ina biashara nyingi sana ambazo zinahusisha mtandao.

Muoenkano Wa Ndani Wa TikTok (Mfano)

Muoenkano Wa Ndani Wa TikTok (Mfano)

Ni wazi kuwa masoko mengi ya usambazaji wa muziki yanapata mapato mazuri tuu ukilinganisha na miaka ya zamani, kampuni nalo limeona lisiwe nyuma katika soko hili.

SOMA PIA  Magwiji ya mitandao ya kijamii yaungana dhidi ya meseji za kigaidi

Kwa sasa fununu zinasema kuwa kampuni hiyo mpya ya masuala ya mziki itakwenda kwa jina la TikTok Music na hapa itawawezesha watu kununua, ku’share’ kucheza na kushusha (download) muziki.

App Ya TikTok

App Ya TikTok

Ndio ni kama masoko mengine ya muziki ambayo tumeyazoea kama vile Apple Music na Spotify sio? Kwa hiyo tutegemee mambo yale yale kama vile kuandaa nyimbo-mtiririko pendwa (play List), uwezo wa ku comment pengine na mambo mengine Zaidi

SOMA PIA  Piga Selfie Na Itumie Kama Emoji Na App Ya Allo!

Ningependa kusika kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je utaweza kuachana na huduma zingine za muziki na kuhamia katika huduma hii mpya?

Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!…

Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii

Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn 

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania