Tumeona makampuni mengi sasa yakiwa yanatafuta njia mbadala za kupata mapato, licha ya sehemu zake za matangazo ambazo tumezizoea, Apple nao waja na hili kupitia App Store.
Ukaichana na kuwa Apple ni moja kati ya makampuni ya kiteknolojia ambayo yanapata mapato mengine sana lakini bado wameona waanze kuonyesha baadhi ya matangazo katika App Store tena katika ule upande wa kipengele cha ‘Today’.

Hili ni moja kati ya soko la Apps ambalo ni kubwa sana na maarufu. Kwa dunia ya leo swala la kuongezeka kwa matangazo katika mtandoa husika sio jambo la kushangaza tumeshaona wengi wa kifanya hivyo
Mitandao mingi sana imeweka huduma mbalimbali za kulipiwa katika mitandao ya kijamii, hii tumeona kutoka kwa WhatsApp Business, Telegram Premium, Snapchat Plus n.k.
Kwa sasa jambo hili liko hatua ya maandalizi kabisa, na hii ni kulingana na vyanzo aminika vinavyosema.

Kumbuka mara ya kwanza kabisa matangazo ndani ya soko hilo yalikua na uwezo wa kutoka katika kipengele cha “You Might Also Like” au ukaona ndani ya App (katika App Store) kwa chini kabisa kuna kilama cha box chenye rangi ya blue kikiwa kimeandikwa Ad.
Ni wazi kuwa matangazo ndio njia kuu ya mapato kwa makampuni mengi ambayo yanaendesha shughuli zao kwa kutumia mtandao (online).

Bila shaka hii ni njia moja wapo kwa kampuni katika kujihakikishia kuwa inapata mapato makubwa tena kwa kupitia App Store.
Vyanzo: MacRumors, 9to5Mac, na AppleInsider.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je hili umelipokeaje? Wewe unaona ni sawa kwa upande wa App store kuanza kuruka kwa matangazo mengi?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!…
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.