fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Teknolojia

Huduma Ya Twitter Blue Yapanda Gharama Za Malipo Ya Mwezi!

Huduma Ya Twitter Blue Yapanda Gharama Za Malipo Ya Mwezi!

Spread the love

Huduma ya kulipia kupitia mtandao wa Twitter inayojulikana kama Twitter Blue ina mambo mengi na ya kuvutia ukilinganisha na Twitter ya kawaida.

Kuna wengi wanaona kamaa Twitter ya kawaida ni mtandao wa kijamii ambao unawatosha kwa kila kitu lakini kuna wengine ambao wanaona ni bora kwenda katika mtandao wa Twitter Blue ambao ni wakulipia.

Twitter Blue

Twitter Blue

Bei ya malipo kwa sasa imepanda kutokea dola 2.99 za kimarekani kwa mwezi mpaka kufikia dola 4.99 za kimarekani kwa mwezi, hili likiwa ni ongezeko la dola 2 nzima.

Kwa ongezeko hili ni kubwa sana lakini kwa wale wapenzi wa dhati wa mtandao huo ni kwamba  bado watakua una uwezo wa kumudu kulipia huduma ya mtandao huu kwa mwezi.

Ongezeko La Bei Katika Mtandao Wa Twitter Blue

Ongezeko La Bei Katika Mtandao Wa Twitter Blue

Lakini vile vile sio lazima kutumia mtandao huu, utaweza kurudi katika mtandao wa Twitter ule wa kawaida na kuendelea kufurahia huduma za Twitter.

SOMA PIA  Go Green; App mahususi kwa ajili kukupa dondoo jinsi ya kutunza vitu mbalimbali

Kwa sasa Twitter Blue inasema kuwa ongezeko hilo la bei litahusisha moja kwa moja kwa wateja wapya. Kwa wateja wa muda mrefu (ambao bado wanaumia huduma hii) kutakua na afadhali kwao—kidogo.

Twitter Blue

Twitter Blue

Ni kwamba kwa wale wa zamani ni bado watalipia kiasi kile kile mpaka mwezi oktoba na kasha baada ya hapo wanaweza wakaamua wenyewe kusitisha huduma hiyo au kuanza kulipia kabla ya wengine.

SOMA PIA  Waanzilishi wa Instagram waacha kazi

Kwa namba nyingine ni kwamba wateja hawa wapewe dirisha la mwezi mmoja ili kuamua kuwa wataendelea na huduma hiyo huku bei ikiwa imeongezeka au lah.

Ningependa kusikia kutoka kwako, je kama ingekua ni wewe unatumia mtandao huu na wakaongeza dola 2 nzima, je ungekua na uwezo wa kuendelea kutumia mtandao huo au ungeachana na huduma hiyo.

Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii

Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn

Hash

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania