fbpx

Facebook ina mbinu ya kuwa karibu na mkufunzi

1

Sambaza

Wakati mwingine unaweza ukafikria kumtumia ujumbe mwalimu/mkufunzi ili upate ufafanuzi wa jambo fulani lakini roho ikasita kwa sababu ya kutokuwa na mazoea ya kutumia njia hiyo ya mawasiliano lakini sasa Facebook imebuni kitu kipya kabisa.

Kwa waliowengi watakuwa wanafahamu kuwa kuna makundi mbalimbali kwenye Facebook na mtu yeyote aliye na akaunti ya Facebook anaweza akatengeneza kundi kwenye mtandao huo wa kijamii. Kundi hilo linaweza kuwa na maudhui ambayo wewe kiongozi utapenda kuyabeba na kuzingatia yanafuatwa.

Katika maboresho yaliyotolewa hivi karibuni na Facebook yanamuwezesha yule mfuatiliaji wa kundi kuwa karibu na kiongozi/mwalimu wake na kuweza kufanya mawasiliano ya faragha ingawani ndani ya kundi, swali ni je, inakuaje?

Kiongozi (admin) wa kundi husika anabuni mada mbalimbali za kujenga/kuelimisha kisha anachagua watu kutoka ndani ya kundi ambao watakuwa ni walimu/wakufunzi na hatimae wanakundi wengine wote wataomba kujiunga kuchangia mada husika na kuwa na uwezo kufanya mazunngumzo ya watu wawili tu.

mkufunzi

Kipengele kipya cha kwenye kundi ndani ya Facebook kinachorahisisha mawasiliano kati ya mwalimu na mwanafunzi wake.

Kipengele hicho hakiruhusu kukiuka miiko iliyowekwa na mtandao husika hivyo kama mambo yanakwenda ndivyo sivyo mtu anaweza akatoa taarifa/akazuia kufanya mazungumzo.

Chanzo: Engadget

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Kuonekana kwa biashara kwenye ramani
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|