Mtoto wa miaka 10 ameshinda shindano ambalo liliandaliwa na wanafunzi wa shahada ya tatu (Uzamivu) kwa kutaka kutengeneza roboti atakayefurahisha jiji la Paris.
Eva mtoto wa Kifaransa mwenye umri wa miaka 10 aliomba kuingia kwenye shindano lililopewa jina “Summer Innovation Fellowship” lililokuwa limeandaliwa na “Digital agency Five by Five” ambalo lilikuwa limelenga wanasayansi wa mambo yanayohusu kompyuta.

Maeneo mabalimbali ya Paris yana huzuni kutokana na majanga yaliyopata miezi kadhaa iliyopita. Anataka atengeneze roboti ambaye atakuwa kivutio katika maeneo mbalimbali ya jiji la Paris-Ufaransa na tayari nimeshaanza kujifuza jinsi ya kutengeneza (coding) roboti katika ” Thymio robots” ingawa kuna changamoto nakutanaznazo kuweza kufanya programu (roboti) hiyo ifanye kazi.
Bi. Kat Borlongan (Mwanzilishi wa Five by Five) amevutiwa sana na kitendo cha mtoto huyo kukubali kuwa anapata tatizo kuweza kufanya roboti huyo afanye kazi aliyokusudia na kuongeza kuwa jambo hilo ni la kishujaa na ndio maana wameamua kuchukua project yake na kumsaidia kufanikisha malengo yake.
Tayari mtoto Eva alishawasiliana msaada Tymio (kampuni inayotengeneza roboti) kuweza kumsaidia kutatua changamoto anazokutananazo kuweza kumfanya roboti huyo afanye kazi.

Mbali na kuomba msaada Eva tayari alikuwa ameshaunda kifaa (3D-printed bigger wheels and a chalk holder) kwa ajili ya roboti wake. Endelea kufuatilia habari mbalimbali kupitia TeknoKona. Daima TeknoKona tupo na wewe msomaji wetu.
Vyanzo: The Telgraph, 3ders.com