Tumezoea kuona tovuti nyingi zikiishia na ‘.org’, ‘.eu’ na ile maarufu kabisa yaani ‘.com’. Sasa na kwa mara ya kwanza karibu miaka 30 iliyopita afrika imepata utambulisho wake wa kipekee katika ulimwengu wa intaneti.
Utambulisho huu wa aina yake ni faraja na habari njema kwa waafrika wote kwani nasi nasi tunaweza kuwa na tovuti yenye “.africa” mwisho. Jambo hili limefanikishwa kwa juhudi na jitihada za Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika anayemaliza muda wake Bi. Nkosazana Dlamini Zuma ambaye pia alishiriki katika uzinduzi huo wa kihistoria.
Uwepo wa “.africa” katika ulimwengu wa intaneti unatoa tafsiri ya kwamba utaunganisha Waafrika katika biashara za mitandaoni, teknolojia. Takwimu zinaonyesha kuwa ni 10.7% ya Waafrika wote ndio wanaotumia intaneti.
Hadi sasa kuna zaidi ya anuani 8,000 za .afrika zimeandikishwa haraka baada tu ya kuanza kupatikana.
DotAfrica itaanza kutumiwa na mtu yetote/kampuni yoyote Afrika kuanzua mwezi Julai.
ZA Central Registry ndio kampuni ya kwanza kuanza kutumia ‘.africa’ ambayo makazi yake yapo nchini Afrika Kusini na. Anuani ya “.africa” itamgharimu mtu/kampuni $18 – 25 tu (Tsh 35,000/= – Tsh 60,000/=) kutegemeana na mtoa huduma.
Kwa hakika sasa itakuwa ni rahisi sana kwa tovuti kutambulika bila hata ya kusoma yaliyomo kwenye tovuti hiyo. Mtu au kampuni itakayotumia anwani ya mfumo wa .africa atatambulika mapema ya kwamba inatoea au inajihusisha na masuala ya bara la Afrika.
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.
Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.
Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|