Idadi kubwa ya watu wamekuwa wakitumia Facebook kama njia mojawapo ya kutangaza biashara/bidhaa zao jambo linalompeleka mtu kufungua ukurasa ambao utakuwa ni maalum kwa kile amabcho atakuwa anakitangaza kwa watu/mashabiki.
Katika njia moja ambayo TeknoKona tunaamini si watu wengi wanaifahamu ni kuweza kubadilisha akaunti ya Facebook kuwa ukurasa badala ya kuwa na akaunti na ukurasa kwa pamoja.
Hatua za kufuata kubadili akaunti binafsi ya Facebook kuwa ukurasa (page).
- Pakua taarifa zako za Facebook. Hii ndio hatua nambari moja itakayokuwezesha kubadili akaunti yako na kuwa ukurasa. Ingia Settings>>Download a copy of your Facebook data>>Start my archive.
Kwa kufuata hatua kwa hatua utaweza kupakuwa taarifa zako za Facebook. - Chagua ‘Admin’ mwingine. Iwapo kuna kurasa ambazo wewe ni moja ya viongozi wakuu (admin) au kama ni wewe tu ndio kiongozi mkuu katika ukurasa huo au kurasa hizo basi itakubidi uchague mtu mwingine atayekuwa admin badala yako la sivyo kurasa hizo zitakuwa hazina kiongozi mkuu.
Sehemu ya kukuwezesha kuchagua nani awe kiongozi wa ukurasa (admin) badala ya mhusika kwa kurasa ambazo anazimiliki/anaziongoza.
- Badili jina na anwani ya makazi. Kutokana na kwamba upo katika harakati za kubadili akaunti yako na kuwa ukurasa wa kibiashara ni vyema ukabadili jina na anwani ili iwe rahisi kwa watu kuweza kutambua kile utakachokuwa ukikitangaza na kukitafutia soko. Ingia Account Settings>>Profile>>Update Information.
Sehemu ya kubadilsha jina na awani ya makazi kwa ajili ya ukurasa wa kibiashara. - Kuhama kutoka akaunti binafsi na kuwa ukurasa. Baada ya kupakua taarifa zako binafsi ya Facebook, ukachagua admin wa kurasa ulizokuwa unaziongoza na kisha kubadili jina/anwani sasa hatua inayofuata ni kubadili akaunti yako na kuwa ukurasa. Bofya –>>HAPA kuhamisha akaunti yako na kuwa page.
Muonekano wa awali katika hatua ya mwazo ya kubadili akaunti binafsi ya Facebook na kuwa ukurasa. - Kukusanya pamoja kurasa zilizojirudia. Inawezekana jina jipya la ukurasa unaotengeneza ambao unatokana na akaunti (profile) yako ya Facebook tayari ukurasa huo upo (majina ya kurasa yanafanana, huo unaotokana na akaunti ya Facebook pamoja na ukurasa mwingine wenye jina sawa na hulo);
Facebook inakupa nafasi ya kuunganisha kurasa hizo mbili na kuwa moja kwa anagalizo: utaweza kuunganisha ukurasa wenye likes chache kwenda kwenye ukurasa mpya (unaotokana na profile yako) na si vinginevyo.
Namna ya kuunganisha kurasa
Nenda kwenye page yenye uliyopadiliisha kutoka akaunti binafsi na kuwa page>>Bofya Edit page>>Update info>>Resources>>Merge duplicates link (link hii inatokea tu iwapo unaongoza page mbili kwa majina yanayofanana)>>Chagua kurasa unazotaka kuziunganisha na kuwa moja.
Ni muhimu kujua kuwa vitu mbalimbali vya kukuwezesha kutoa taarifa zako kutoka kwenye akaunti (profile) kwenda kwenye ukurasa vitapatikana siku 14 baada ya ukurasa kubadilishwa. Fanya maamuzi sasa.
Vyanzo: Jon Loomer, mitandao mbalimbali.
One Comment
Comments are closed.