fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Android apps iOS Teknolojia

Mazungumzo ya WhatsApp: Hamisha kutoka Android kwenda iOS

Mazungumzo ya WhatsApp: Hamisha kutoka Android kwenda iOS

Spread the love

Suala la kuweza kuhamisha mazungumzo ya WhatsApp kutoka kwenye iOS kwenda Android sio shaka tena kwani inawezekana! Kama hilo limewezekana basi hata upande wa pili wa (kutoka Android kwenda iOS)shilingi pia mambo yanapikika.

Kwa sababu moja au nyingine unaweza ukawa unamiliki simu janja ambazo zinatumia programu endeshi mbili tofauti kwa maana ya Android na iOS. Vilevile, inawezekana kabisa hutaki kupoteza mazunguzo yako ya WhatsApp iwapo utaamua kuanza kutumia WhatsApp ya kwenye iOS na hapo ndipo unapowaza nini cha kufanya ili ukihmia upande wa pili hupotezi vitu vyako vya muhimu kwenye WhatsApp.

SOMA PIA  YERKA - Ifahamu Teknolojia ya Baiskeli 'Isiyoibika'

Kwa habari zilizopo mara baada ya zoezi la kuweza kuhamisha mazungumzo ya WhatsApp kutoka iOS kwenda Android sasa shilingi imegeuzwa upande wa pili na kazi inafanyika kumuwezesha mtumiaji mwenye simu janja ya Android anapotaka kutumia WhatsApp kwenye iPhone.

Android kwenda iOS

Uwezekano wa kuhamisha mazungumzo ndani ya WhatsApp kutoka kwenye simu ya Android kwenda iPhone.

Zoezi hilo ambalo bado lipo kwenye hatua ya majaribio inaelezwa kuwa linawezekana kwa kutumia waya maalum ambao unaunganishwa kwenye simu janja husika ili kufanikisha kile ambacho kimekusudiwa.

Ni ngumu kusema lini suala hilo litawezekana kwa watumiaji wote wa WhatsApp lakini kama kitu hicho kipo kwenye hatua ya majaribio basi huenda tukakiona katika siku za usoni.

Chanzo: WaBetaInfo

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania