fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Samsung simu Teknolojia

Simu janja Samsung Galaxy M52 5G ipo karibu kutoka

Simu janja Samsung Galaxy M52 5G ipo karibu kutoka

Spread the love

Moja ya simu janja ambazo zinatazamiwa kutoka katika siku za usoni Samsung Galaxy M52 5G kwani tayari imeshaanza kuonekana kwenye tovuti za kuaminika.

Mwezi Septemba una mengi kutoka kwa makampuni yanayojishughulisha na biashara ya simu janja. Hivi karibuni tutegemee kuiona Samsung Galaxy M52 5G kwenye macho yetu ikiwa tayari kuja kwa wanunuzi. Maneno haya yanakuja mara baada ya rununu husika kuonekana kwenye tovuti ya Samsung huko India.

SOMA PIA  Kamera Ya Mbele (Selfie) Mbioni Kutumika Kama 'Password' Ili Kuweka Ulinzi Zaidi!

Hatua hiyo inatoa tafsiri kuwa ujio wa simu janja hausika wala haupo mbali bali ni suala la muda tuu lakini wakati wake wa kuja umesalia kidogo na ulimwengu utapata kuzifahamu sifa za rununu inayozungumziwa.

Galaxy M52

Muonekano unaoamikika kuwa wa Samsung Galaxy M52 5G.

Sifa zake je?

Kuna machache ambayo SI RASMI yanahusisha sifa za simu jasnja husika. Simu hii inaaminika kuwa na kioo chenye urefu wa inchi 6.7 ubora wa AMOLED, kamera kuu ina MP 64 huku injini ikiwa ni Snapdragon 778G lakini pia programu endeshi ni Android 11 ikiwa sambamba na UI 3.1 na kwa upande wa betri ni 7000mAh kama ilivyo kwa mtangulizi wake; Galaxy M51.

Galaxy M52

Sura ya mbele ya inayoaminika kuwa ni Samsung Galaxy M52 5G.

Simu janja husika inatazamiwa kugharimu kuanzia $295.46|zaidi ya Tsh. 679,558 kwa bei ya ughaibuni lakini hizi ni taarifa za chini kwa chini tuu. Tutafahamu kitukila kuhusiana na simu hii siku itakapozinduliwa.

Kumbuka kufuatilia TeknoKona ili uweze kuhabarika halikadhalika kuelimika kuhusu teknolojia.

Vyanzo: GSMArena, mitandao mbalimbali

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania