Facebook imekuwa ikibiresha vitu mbalimbali na kwa namna moja au nyingine akaunti hiyo haipendezi bila kuwa na machapisho ya picha kutoka kwa marafiki kwenye mtandao huo wa kijamii.
Sote tunafahamu vyema kuhusu vitu ambavyo vinarushwa kwenye Facebook, vinaweza kuwa katika mfumo wa maandishi pekee au picha/picha jongefu pamoja na maelezo sasa imefahamika kuwa Facebook wapo njiani kuleta uwezo wa kuongeza muziki kwenye picha/picha mnato unayotaka kuichapicha.
Kwa lugha rahisi ni kile ambacho utakuwa umekirusha (picha/video) itakuwa na kuambatanisha na muziki ambao yule atayeona chapisho lako atakuwa na uwezo wa kubofya na kusikiliza.
Kitu hicho unaweza kuwa umeshakiona kwenye kipengele cha stories kwenye Facebook lakini sasa kinaletwa kwenye uso wa mbele (News Feed).
Utafanyaje kufanikiwa kuchapisha picha/video ikiwa na muziki?
Wakati umeshafanikiwa kuweka picha/picha mnato kutoka kwenye kifaa chako kwenda kwenye Facebook utabofya kwenye alama ya stickers kisha utabonyeza alama ya muziki kisha utachagua kipande cha muziki ambao utaupenda kurusha kwenye akaunti yako ya Facebook.
