fbpx
Facebook, Udukuzi, Usalama

Data za akaunti milioni 210 za Watumiaji wa Facebook zavuja

data-za-akaunti-milioni-210-za-watumiaji-wa-facebook-zavuja
Sambaza

Data za akaunti milioni 210 za watumiaji wa mtandao wa Facebook zavuja baada ya kudukiliwa na taarifa za akaunti zao zinapatikana kwa urahisi mtandaoni.

Jumla ya data zilizowekwa wazi zinaonesha ni data zinazohusisha akaunti milioni 419 ila msemaji wa Facebook amesema baada ya kuzipitia wamegundua ni milioni 210 tuu na huku akidai data hizo nyingi zake ni za akaunti za zamani, na nyingine zimerudiwa – zinahusisha akaunti zile zile.

Data za watumiaji wa facebook zavuja
Unashauriwa kufanya mabadiliko ya nywila zako mara kwa mara

Data hizo zimehusisha taarifa muhimu kuhusu watumiaji wa Facebook kama vile anuani za akaunti zao, namba zao za simu na pia kwa baadhi ni majina yote ya muhusika.

INAYOHUSIANA  Facebook au Twitter: Ipi Ilishinda Kombe la Dunia?

Data hizo zimehusisha watumiaji wa Marekani zaidi – ambapo akaunti milioni 133 kati ya 210 zilikuwa za watumiaji wa nchi hiyo. Huku milioni 50 zikiwa za watumiaji kutoka Vietenamu, huku milioni 18 zikiwa za Waingereza. Udukuzi huu umechukua sifa ya kuwa moja ya udukuzi mkubwa zaidi wa data duniani – kwa idadi ya watumiaji.

Tayari Facebook na makampuni mengine makubwa ya kimtandao kama vile Google na Amazon wamejikuta kwenye hali ya kuangaliwa kwa jicho la ukali na umakini zaidi na vyombo vya usalama wa data za watumiaji wa huduma zake. Vyombo vya serikali ya Marekani na ata barani Ulaya zishazipiga faini kubwa kwa ukiukwaji wa usalama wa data za watumiaji wa huduma zao. Umoja wa Ulaya (EU) umetoa onyo kali baada ya taarifa hizi kutoka, uchunguzi unaweza kufuata.

INAYOHUSIANA  Facebook ina mbinu ya kuwa karibu na mkufunzi
facebook sheria
Vyombo vya kisheria vya barani Ulaya na Marekani vimekuwa vikali sana siku hizi dhidi ya makampuni kama Google na Facebook. Ni kawaida makampuni haya kupigishwa faini za mabilioni ya pesa kwa kukiuka au kufanya uzembe katika eneo la data za watumiaji au tabia zisizo nzuri kiushindani katika biashara. Google wanashikilia rekodi kubwa ya faini kuwahi kulipwa barani Ulaya.

Taarifa hii imekuja wakati mbaya kwani tayari Facebook wanapata pingamizi la kiaina kutoka bunge la Marekani (Congress) kuhusu wazo lao la kuja na sarafu yao ya kidigitali – libra. Kama hawawezi kulinda data za watumiaji wao wa mtandao wa kijamii kama Facebook inaweza ikawa hatari kupewa nafasi katika sekta ya fedha.

Tayari bunge la Marekani limeandaa mswada unaokwenda kwa jina la ‘Keep Big Tech Out of Finance Act’, yaani ‘Kuweka makampuni makubwa ya sekta ya teknolojia nje ya sekta ya fedha’ – lengo likiwa ni kuyazuia makampuni kama Google, Facebook na Amazon kuingia kwenye sekta ya huduma za kifedha.

INAYOHUSIANA  Muonekano Mpya wa Facebook kwa watumiaji wa Kompyuta

Ili kuwa salama na huduma za kimtandao Teknokona inakushauri kufanya mabadiliko ya mara kwa mara ya nywila katika tovuti na app mbalimbali unazotumia.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |