fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

tecno

Intaneti Tanzania Tigo

Mabadiliko ya Vifurushi Tigo – Bei ya Vifurushi vya Intaneti ‘Yapaa’

Mabadiliko ya Vifurushi Tigo – Bei ya Vifurushi vya Intaneti ‘Yapaa’

tecno

Kuna mabadiliko ya vifurushi kwenye mtandao wa Tigo ambayo yameleta malalamiko mengi kutokana na kuwa ya makubwa katika ushushwaji wa viwango vya GB ambavyo mtu anapata kwa malipo ya kwa siku, wiki na mwezi.

Tigo hawatatoa maelezo yeyote kuelezea sababu ya mabadiliko haya ya vifurushi lakini ni mabadiliko makubwa sana ya bei na thamani ya GBs ambazo mtu anazipata anapolipia.

Kwa mfano ni siku chache tu nyuma nilijiunga kifurushi cha mwezi kwa gharama ya shilingi 20,000/= na nilipata GB 16 za kuweza kutumia kwa kipindi cha siku 30. Je shilingi 20,000 inakupatia GBs ngapi sasa kwa ajili ya kipindi hicho hicho cha mwezi? – GB 9. Kwa punguzo la GB 7 hii ina maanisha ni punguzo la gbs la kwa zaidi ya asilimia 40.

vifurushi vya tigo Mabadiliko ya Vifurushi Tigo

Mabadiliko ya Vifurushi Tigo – Siku chache zilizopita uliweza kupata GB 4 za kutumika ndani ya siku 7 kwa Tsh 5,000/= na GB 16 kwa Tsh 20,000/= kwa ajili ya kutumika ndani ya siku 30

 

Kutoka 2,000/= kukupa 2.5GB hadi kukupa 1GB kwa siku.

SOMA PIA  Afrika yapata utambulisho wake(".africa") baada ya miongo mitatu

Vifurushi vipya

Mabadiliko ya Vifurushi Tigo

Bei ya Vifurushi vya mwezi kwa sasa

 

Mabadiliko ya Vifurushi Tigo

Bei ya vifurushi vya wiki kwa sasa

 

Kwa muda mrefu huwa tunategemea mabadiliko makubwa ya gharama za maongezi na bidhaa nyingine mbalimbali katika kipindi cha bajeti za kiserikali au kukiwa na taarifa za aina mpya za tozo dhidi ya mitandao ya simu.

SOMA PIA  VLC haipatikani kwa baadhi ya simu za Huawei

Je mabadiliko haya ya gharama za huduma ya intaneti kutoka Tigo yatakuwa yamesababishwa na nini? Tutaendelea kufuatilia lakini kama jambo ni la uhakika ni kwamba watanzania wengi wanamiliki laini zaidi ya moja na uamuzi huu wa Tigo unaweza sababisha wakapoteza wateja wengi kwenye huduma ya intaneti na kujikuta katika hali ya kufanya mabadiliko tena ya vifurushi hivi.

vifurushi vya tigo

Tatizo moja kubwa linaloonekana kuwepo kwa sasa ni uhuru wa mitandao ya simu kubadilisha gharama hizi bila kutoa muda wa kutosha wa kuwataarifu wateja wao kuhusu mabadiliko yanayokuja. Hii ni sehemu ambayo TCRA wanawajibu wa kupasimamia vizuri – Picha ni ya post kutoka Twitter https://twitter.com/YayaThatFemale/status/1354261716817817600 

 

Kwa kuwasaidia wengine, ebu tuambie ni mtandao gani mwingine wa simu una vifurushi vya bei nafuu zaidi vya siku/wiki na mwezi ukilinganisha na bei ya vifurushi vya intaneti vya sasa?

Comrade Mokiwa

Comrade Mokiwa

Muanzilishi wa Teknokona na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania