fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

tecno

Afya

Kipimo cha Covid19 kupitia njia ya haja kubwa chaleta taaruki

Kipimo cha Covid19 kupitia njia ya haja kubwa chaleta taaruki

tecno

Maongezi katika mitandao ya kijamii nchini China yapamba moto baada ya kipimo cha Covid19 kinachohusisha njia ya haja kubwa kutambulika kama njia nyingine rasmi ya upimaji wa Covid 19 hasa hasa kwa watu ambao wanawekwa chini ya uangalizi – yaani quarantine.

Vyombo vya habari vya kiserikali vimeanza kuitambua rasmi njia hiyo mpya ya upimaji wa virusi vya COVID.

Kipimo cha Covid19 kupitia njia ya haja kubwa

Kipimo cha Covid19

Kwa nini kuwa na kipimo cha Covid19 kupitia njia ya haja kubwa?

Wanasayansi wa nchini humo wametetea kipimo hicho kwa sababu kuu mbili

  • Kwa vipimo vya njia ya sasa, kooni na puani, inaonekana ni rahisi vipimo hivyo kuonesha mtu yupo sawa pale hali ya virusi vya kovidi ikiwa chini. Mfano watu waliokuwa wapo kwenye hatua za mwisho za kupona vipimo hivyo vilionesha ya kwamba hawana virusi hivyo tena, ila vipimo vilivyohusisha kuchukua sampuli kutoka kwenye njia ya haja kubwa vikaonesha bado watu hao wana virusi vya mafua ya korona.
  • Kipimo hichi si lazima kwa watu waohisiwa. Ni muhimu zaidi kwa watu wanaohifadhiwa kwa ajili ya uangalizi – yaani quarantine.
SOMA PIA  Chanjo ya Korona /Covid19 kuanza kutumika Uiengereza

Ni mwaka sasa tokea China iwe taifa la kwanza kuanza kupambana na virusi hivi. Tayari limeanza juhudi kubwa za ugawaji chanjo huku wakiwa na lengo la kuwapatia chanjo raia wake milioni 50 kabla ya mwaka mpya wa kichina kuingia hivi karibuni.

SOMA PIA  Viwanda vya kampuni ya Louis Vuitton kutengeza visafisha mikono

Je una mtazamo gani juu ya kipimo hichi?

Vyanzo: WashingtonPost na vyanzo mbalimbali
Comrade Mokiwa

Comrade Mokiwa

Muanzilishi wa Teknokona na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania