fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

tecno

Afya Teknolojia

Upimaji Tezi Dume kwa kupitia mkojo wafanikishwa kwa kutegemea teknolojia ya AI

Upimaji Tezi Dume kwa kupitia mkojo wafanikishwa kwa kutegemea teknolojia ya AI

tecno

Upimaji tezi dume umekuwa ni moja ya jambo ambalo bado limekuwa likifanywa kwa njia ambayo imewafanya wanaume wengi kutokuwa na mwamuko katika upimaji wa tatizo hilo la afya. Hii ni kwa kuwa njia ya sasa inahusisha daktari kuingiza kidole katika kuta za njia ya haja kubwa, jambo hili linaweza likawa la kihistoria kwa msaada wa teknolojia ya AI.

upimaji tezi dume

Timu hiyo ya wanasayansi ni ya Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Korea Kusini (Korea Institute of Science and Technology (KIST)). Utafiti huo ulipatiwa fedha na wizara ya Sayansi na Tehama ya nchini humo. Timu hiyo iliongezwa na Dk. Kwan Hyi Lee wa Biomaterials Research Center na Profesa In Gab Jeong wa Asan Medical Center

 

SOMA PIA  Project BLAID - Toyota waja na Kifaa kusaidia Wasioona Kutembea bila Msaada

Wanasayansi nchini Korea Kusini wamefanikiwa kutengeneza kifaa cha upimaji wa tezi dume kwa kupima mkojo. Kipimo hicho kinaendeshwa na teknolojia ya kompyuta kwenye mfumo wa AI (Artificial Intelligence).

Wanasayansi hao wamesema ili kuweza kutengeneza kifaa hicho chenye uwezo wa kupata matokeo sahihi kwa takribani asilimia 100 umehusisha kuipa kompyuta uwezo wa kupima mamia vitu kwenye mkojo ili kuipa uwezo wa kuja na matokeo ambayo yanakuwa yana usahihi kwa kiwango kikubwa.

Njia maarufu ya upimaji tezi dume imekuwa ni moja ya changamoto kwa wanaume wengi kujitokeza kufanya kipimo hicho

AI imewezaje kutumika?

AI ni mfumo wa akili bandia ya kompyuta inayokuwa na uwezo wa kuchambua data kwa urahisi na uharaka. Ili kuwezesha vifaa hivi kuwa na uwezo wa kupata matokeo yaliyosahihi tena ndani ya dakika ishirini tuu watafiti hao wameipa mashine data za kiafya za watu wenye matatizo ya tezi dume na data za kiafya za watu wasio na matatizo ya tezi dume, kwa kutumia data hizo kompyuta inapopima mkojo inafanya uchambuzi chembe zote za kibaiolojia zilizopo kwenye mkojo kwa kulinganisha data hizo zingine.

SOMA PIA  TTCL Kuboresha Huduma, Wanakuja na 4G LTE

Ni kwa miaka mingi wanasayansi wamekuwa wakikuna vichwa na kufanya tafiti mbalimbali za kutafuta njia nyingine ya upimaji wa tezi dume.

Tafiti hiyo tayari imeanza kuchapishwa kwenye majarida ya tafiti za masuala ya kitabibu, hili ni jambo zuri kwani itaruhusu watafiti wengine pia kuanza kushiriki katika uchambuzi wa matokeo hayo kabla ya hatua za utengenezaji wa kwa wingi na kuanza kupatikana kwa vipimo hivyo katika vituo vya afya.

Vyanzo: eurekalert.org na vyanzo mbalimbali
Comrade Mokiwa

Comrade Mokiwa

Muanzilishi wa Teknokona na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania