Kipengele cha ‘Optimized Battery Charging’ kinafanya MackBook zijaze chaji kwa haraka mpaka kufikia asilimia 80 na kisha chaja inakua haiingii tena. Hata hivyo kipengele hichi sio cha ajabu sana maana kina maana kubwa.
Sawa inaweza ikawa inashangaza hivi lakini Apple wamesema sio vizuri kwa mabetri ya lithium-ion kuchajiwa mpaka kufikia asilimia 100 na kuendelea kukaa katika chaja kwa asilimia 100 (mara nyigi hii huwa inatokea usiku).
Kinachofanyika ni kwamba betri inajaa mpaka kufikia 80% na 20% zingine zinaingia taaratibu endapo simu itakua imeshasoma tabia na mwenendo wako (mfano muda wa kulala mpaka kufikia kuamka).
Sasa basi kama hupendi hiki kipengele au ungependa MacBook yako iwahi kujaza betri mpaka kufikia 100% unaweza kuzima kabisa huduma hii katika system preferences au unaweza ukaamuru kujaa mpaka asilimia 100 wakati ukiwa unachaji.
-
NJIA YA KWANZA
Hii ni njia nyepesi zaidi ya kuwezesha MacBook yako kujaa mpaka kufikia asilimia 100 kwa urahisi zaidi.
Wakati ukiwa unachaji MacBook yako nenda katika ufito wa menu. Ingia katika alama ya betri linalojichaji na kisha chagua “Charge to Full Now”

Kama hilo neno hujaliona katika listi basi bofya kitufe cha ‘Option’ huku uki’click’ alama hiyo ya betri
Mpaka hapo Macbook yako itaanza kujichaji mpaka asilimia 100 kwa uharaka zaidi
-
NJIA YA PILI
Njia hii ya pili ni ile ya kufuta kabisa na hapa inabidi u’click’ logo ya Apple kule juu kushoto kabisa na kisha kwenda katika “System Preferences”
Ukishaingia, nenda kwenye betri

Ukiashafika, hakikisha kuwa kipengele cha “Optimized Battery Charging” unakizima, utapokea ujumbe ambao unakuuliza uzime kipengele hicho mpaka kesho yake tuu au unataka kukizima kabisa, unaweza ukachagua kulingana na chaguo lako.

Mpaka hapo MackBook yako itaweza kuachaji betri mpaka kufikia asilimia 100 kwa kutumia muda mchache sana ukilinganisha na wakati ambapo kipengele hichi kilivyokuwa kimewashwa.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika uwanja wa maoni
Kumbuka Kutembelea TeknoKona Kila Siku Kwani Daima Tupo Katika Teknolojia!
No Comment! Be the first one.