Kwa teknolojia ya simu ilipofikia bado Xiaomi kutoka nchini china inaonyesha kuwa bado inapambana sana ili kuhakikisha kuwa inabaki katika nafasi za juu kabisa katika soko la simu na vifaa vyake.
Mwaka jana (2020) mnamo mwezi october iliweza onyesha simu ikitoka asilimia 0 mpka asilimia 100 ndani ya dk 19 wakati ikiwa inachajiwa.
Kwa sasa wameweka rekodi kwa simu yao ya Xiaomi MI 11 Pro ambayo ilikua na maboresho kidogo na betri la 4,000mAh, betri hilo limeweza kujaa chaja kutoka 0% mpaka 100% ndani ya dk 8 tuu.
Hii imekua ni rekodi mpya kwao, simu imetoka asilimia 0 mpaka 10 ndani ya sekunde 44 na kufika mpaka 50% ndani ya dakika 3. Mpaka inamalizika kujaa kabisa ilitumia dakika 7:57.
Tweet kutoka Xiaomi
⚡200W Wired Charging
⚡120W Wireless ChargingWe're about to redefine the charging experience with #XiaomiHyperCharge. #InnovationForEveryone pic.twitter.com/2rPrzw7BEu
— Xiaomi (@Xiaomi) May 31, 2021
Fununu ni kwamba kifaa (chaja) hiki kinajulikana kama ‘Xiaomi Hyper Charge’ japokuwa hakuna taarifa kamili kwamba kitatoka lini. kitaanza uzwa lini na taarifa zake zingine zikiwa zimewekwa kama siri.
Charge up to 100% in just 8 minutes using wired charging and 15 minutes wirelessly! #XiaomiHyperCharge
Too good to be true? Check out the timer yourself! #InnovationForEveryone pic.twitter.com/muBTPkRchl
— Xiaomi (@Xiaomi) May 31, 2021
Kumbuka kwa teknolojia ya kuchaji simu janja kwa haraka ambayo tunaitumia sasa bado haifikii teknolojia hii ambayo Xiaomi wameionyesha kwa uharaka wa kuchaji simu
Siku ambayo teknolojia hii ikiwa imeingia katika soko, itakua na msaada mkubwa sana na kampuni inaweza ikajizolewa hela nyingi kwa kuuza vifaa vinavyotumia teknolojia hii.
No Comment! Be the first one.