fbpx

Apple, Gari, Magari, Teknolojia, Tesla

Elon Musk: “Tulijaribu kuwauzia Apple kampuni nzima ya Tesla ila Tim Cook akazingua”

elon-musk-apple-tesla-ila-tim-cook-akazingua

Sambaza

Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya magari yanayotumia mfumo wa umeme ya Tesla, amesema walishajaribu kuwauzia Apple kampuni ya Tesla ila Tim Cook alizingua. Inasemekana kwa wakati huo kampuni ya Tesla ilikuwa kwenye changamoto mbalimbali.

Tim Cook, Mkurugenzi Mkuu wa Apple

Kama Apple wangekubali kufanya mazungumzo na Bwana Elon Musk na kununua kampuni hiyo basi wangekuwa kifua mbele kwenye teknolojia ya magari, kampuni ya Tesla ina thamani ya mara 10 zaidi ukilinganisha na bei ambayo Elon Musk alitaka kuwauzia kipindi hicho.

SOMA PIA  Samsung Hizi Ndio Zinazokubali Teknolojia Ya "Wireless Charging"!
Elon Musk
Mwanzilishi wa makampuni ya SpaceX, Solar City na Mkurugenzi wa kampuni ya Tesla

 

Inasemekana tayari Apple wameaanza uwekezaji ili kujiingiza katika biashara ya utengenezaji na uuzaji wa magari ya kisasa yanayotumia Umeme. Ila kwa sasa tayari Tesla ndio kampuni iliyo juu zaidi kwenye teknolojia hiyo, ikitoa ushindani mkubwa ata kwa makampuni mengine makubwa ya muda mrefu kama vile Toyota na General Motors.

Tayari app wanaprogramu yao kwa ajili ya magari. Programu hii inayokuwezesha unganisha simu ya iPhone pamoja na gari inapatikana kwenye magari ya hadhi ya juu.

 

Kulingana na taarifa za chombo cha habari cha Reuters, Apple wanategemea kutambulisha gari lao la kwanza ifikapo mwaka 2024. Kama watafanikiwa au hapana, bado ni mwanzo sana kufahamu kwa kuwa ndio kwanza vyanzo vya uhakika vimeanza kutoa taarifa juu ya malengo hayo ya Apple.

Kampuni ya Tesla kwa sasa tayari imejiweka vizuri kwenye soko na inatambulika kama kampuni iliyo na teknolojia za kisasa katika mfumo mzima wa magari yake – uwezo wa kwenda kilometa za mbali kwa kuchaji, uwezo wa kujiendesha yenyewe bila uhitaji wa dereva nk.

SOMA PIA  NASA kuchunguza sampuli za sayari! #Sayansi

Hakika itakuwa mkurugenzi wa Apple, Bwana Tim Cook anajutia kiasi flani uamuzi wake wa kutokubali kikao na Bwana Elon Musk pale alipoonesha nia ya utayari wa kuuza kampuni ya Tesla kwao miaka kadhaa nyuma.

Chanzo: Yahoo

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Sambaza
Tags: , ,

Comrade Mokiwa

Comrade MokiwaMuanzilishi wa Teknokona na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COMMuda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.| mhariri@teknokona.com |

Toa Maoni

Your email address will not be published. Required fields are marked*