Kiongozi wa upinzani kutoka chama cha wafanyakazi nchini Uingereza, Bw. Jeremy Corbyn ameshauri kuwa makampuni nguli yaongeze kodi na kutumika kulipia tozo mbalimbali ili kuwapunguzia mzigo wa kodi wananchi wa hali ya chini.
Bw. Corbyn ameshauri tozo kwa leseni mpya ambayo itakuwa ni mbadala kwa ile ya sasa akiwalenga makampuni yanayotoa huduma za intenti, mitandao ya kijamii na nyingine zote ambazo zinapata faida kubwa.
Bw. Jeremy Corbyn-Kiongozi machachari kutoka chama cha wafanyakazi nchini Uingereza.
Je, kitakachopatikana kitatumika wapi?
Kwa mujibu wa kiongozi huyo kutoka chama cha wapizani kodi hiyo itatumika kulipia huduma ya wananchi kupata matangazo ya shirika la habari BBC (British Broadcasting Corporation) ambapo kwa mwaka mwananchi anapaswa kulipia $192 ili kuweza kuangalia chaneli/kurekodi kipindi kinachorushwa mubashara kinachoonyeshwa kwenye chaneli hiyo.
Mpaka mwisho wa mwaka 2017 BBC iliweza kupata kiasi cha Pauni 3.7bn zizlizotokana na malipo kutoka kwa wananchi.
Bw. Jeremy Corbyn anaamini bila kuongezea kodi kuwa juu makampuni hayo itafikia kipindi sekta ya habari (mitandao ya kijamii) itakuwa haishikiki kwa kupata faida kubwa halafu wananchi wa hali ya chini wakibaki kuteseka.
Vyanzo: Reuters, The Guardian
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.
Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.
Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|