fbpx

Nokia 8110 yenye teknolojia ya kisasa

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Nokia wanaonekana kutosahau simu zao za zamani kwani kwa mara nyingine ameamua kuirudisha Nokia 8110 kwaenye ulimwengu wa sasa lakini ikiwa na teknolojia ya kisasa.

Kwa ambao wamekuwa ni wapenzi wa simu za Nokia tangu miaka ya nyuma mpaka hivi leo simu ya Nokia 8110 sio ngeni kwao. Kwa ufupi tu, ni simu ambayo kwa mara ya kwanza ilitoka mwaka 1996 na kuweza kutumiwa kwenye sinema ya “The Matrix.

teknolojia ya kisasa

Nokia 8110 ya mwaka 1996 kwenye sinema ya “The Matrix”.

Nokia 8110 ina kipi kizuri/cha kisasa?

Intaneti. Simu hii inatumia teknolojia ya 4G kwenye intaneti na ni kitu tofauti kidogo kulinganisha na Nokia 3310 ambayo ilitoka toleo la 2G/3G kisha baadae ikatoka ambayo inatumia 3G pekee.

INAYOHUSIANA  Asus Zenfone 6: Simu ya kamera mbili kwa moja

Kamera. Simu hiyo ina kamera ya kawaida lakini picha zake ni ang’avu kiasi cha kuridhisha. Haina kamera ya mbele lakini ile ya nyuma ina 2MP pamoja na kuweza kutoa mwaga (LED flash).

teknolojia ya kisasa

Muonekano wa picha iliyopigwa kwenye Nokia 8110.

RAM/Memori ya ndani. Ili kuendana na soko kwa simu ya kawaida kama Nokia 8110 itakuvutia kwa sababu ina uwezo wa kuhifadhi vitu ya mpaka GB 4 na kuweza kuweka memori ya ziada mpaka GB 32. RAM yake ni 512MB.

Sio ya mguso. Waswahili wana msemo “Jasiri haachi asili”, maneno haya yana ukweli ndani yake kwa toleo la Nokia 8110 mwaka 2018 kwani imebaki vilevile kwa kuwa na kicharazio kama ilivyokuwa toleo la mwaka 1996.

teknolojia ya kisasa

Nokia 8110 toleo la mwaka 2018 na zipo za aina mbili; zinazotuia kadi moja kwenye simu huku nyingine zina uwezo wa kutumumia laini mbili.

Mengineyo kuhusu Nookkia 8110.

Kwenye simu hiyo pia utaweza kutumia huduma ya Google Map, Youtube, WiFi, GPS, FM Radio, Bluetooth, USB 2.0, kipuri mama ni Qualcomm Snapdragon 205 yenye kasi 1.1GHz, programu endeshi ni KaiOS, kioo chake kina urefu wa inchi 2.4, inapatikana katoka rangi Nyeusi/Njano na uzito wake ni gramu 117.

teknolojia ya kisasa

Sehemu ya kicharazio unaweza ukaifunika/kuifunua vilevile kupokea na kujibu jumbe zilizotumwa kwenye barua pepe, ni baadhi tu ya sifa za Nokia 8110.

Uwezo wake wa kukaa na betri ndio wa kusisimua kwani inaelezwa kuwa inaweza kutunza umeme mpaka siku 25 kwa matumizi ya kawaida na bei yake ni $88|zaidi ya Tsh. 200,000.

Vyanzo: The Guardian, Engadget

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.