fbpx

Kilimo kinachotumia teknolojia zaidi

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Kilimo cha siku hizi kimekuwa na changamoto za hapa na pale lakini kwa ambao wameshaweza kutumia fursa ya uwepo wa kilimo cha kisasa wamekuwa wakinufaika kutokana na kutumia teknolojia zaidi.

Tatizo la vijana kukimbilia mijini kutafuta kazi nyingine za kufanya na kuacha ardhi yenye rutuba vijijini limekuwa ni tatizo ambalo linasumbua nchi nyingi duniani. Kwa kikubwa teknolojia imeonekana kuwa msaidizi kwa vitu vingi na kwa hili pengine likawavutia wakulima:

INAYOHUSIANA  Jinsi Ya Kuhamisha App Na Taarifa Zingine Kutoka Simu Moja Kwenda Nyingine!

Matumizi ya ndege zisizo na rubani (drones) zimekuwa zikitumiwa na wakulima wa mpunga nchini Japan. Kilimo hicho kinatumia ndege kumwaga dawa shambani kwa ajili ya kukinga dhidi ya magonjwa/wadudu waharibifu.

teknolojia zaidi

Ndege isiyotumia rubani ikiwa kazini.

Kwanini matumizi ya ndege zisizo na rubani zimekuwa kivutio?

Wakulima wengi Japan wana umri wa miaka 67-68 kwa wastani na kutokana na ukweli kwamba nguvu za watu wenye umri huo zimepungua lakini  ndege isiyokuwa na rubani inaweza kunyunyuzia dawa/mbolea shamba zima la mpunga kwa muda wa robo saa; iwapo  uktumia rasilimali watu kufanya kazi hiyo ingechukua zaidi ya saa moja kumaliza kazi hiyo.

INAYOHUSIANA  Vitu vya Kufikiria katika Kununua Laptop kwa Matumizi ya Mwanafunzi

Ndege hizo zinaweza kuongozwa ka kutumia tabiti (iPad) na programu wezeshi ya ramani ambayo ni rahisi kuielewa na kuitumia hivyo anachohitaji mkulima ni kukaa sehemu na kuongoza kifaa hicho.

teknolojia zaidi

Mkulima wa mpunga nchini Japan akiongoza ndege isiyokuwa na rubani kwa ajili ya kazi za shamba.

Bei yake sio rahisi….

Ndege hiyo kukamilika kwa ajili ya kazi za kilimo inagharimu $135,758|Tsh. 312,243,400. Ni fedha nyingi lakini kwa Japan makampuni mbalimbali yanatoa huduma hiyo (kilimo cha kutumia ndege isiyokuwa na rubani) lakini kw malipo fulani.

teknolojia zaidi

Teknolojia hiyo inaweza kutoa mwongozo wa kiasi gani cha dawa/mbolea kinahotajika na hatimae wakulima kuweza kukadiria mavuni yao.

Waafrika/Tanzania tukithubutu tunaweza na vijana wataacha kukimbilia mijini wakitafuta kazi nyingine za kufanya.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.