Kama ni mtumiaji mzuri wa mtandao wa Instagram ni wazi kuwa utakua unajua kwamba kuna aina za Akaunti kwenye mtandoa huo. Hizi si zingine bali kuna ile ya kawaida kabisa yaani Personal, Business na ile ya Creator.
Akaunti hizi zote zina matumizi tofauti kwani hazifanani moja kwa moja. Ni wazi kuwa akaunti hizi ili uwe nazo inategemea na kazi ambayo unataka kuifanya katika mtandao huo. Leo TeknoKona inakujuza tofauti kati ya akaunti hizi tatu katika mtandao wa instagram.
Maana Ya Akaunti Ya ‘Personal’ Katika Mtandao Wa Instagram!
Akauti hii ni ile ya kawaida kabisa ambayo kila mtu anaipata mara tuu baada ya kujiunga katika mtandao huu. Hii inamaana kawamba ni ile akaunti ambayo inakuwa kabla ya mtumiaji kuibadilsha kwenda katika aina zingine za akaunti (business na creator).
Uzuri wa aina hii ya akaunti ni kwamba unaweza ukaweka ukurasa wako katika mtandao huu ukawa wa kibinafsi zaidi (private) hii inamaanisha hata mtu akikufollow itabidi kwanza umkubalie ombi lake ndio aweze kuona vitu unavyoposti katika ukurasa wako.
Bila hivyo hii inamaanisha kwamba hatoweza kuona kitu ambacho umetuma katika mtandoa huo. Hii imekaa Poa sio?

Maana Ya Akaunti Ya ‘Business’ Katika Mtandao Wa Instagram!
Akaunti za aina hii zimeundwa mahususi kwa ajili ya biashara mfano, saluni, wanaofanya biashara za mtandao n.k.
Uzuri wa aina hii ya akaunti ni kwamba utaweza kufanya kila kitu ambacho personal account inafanya na pia utakuwa na vitu vya ziada vya kufanya navyo ni kama ifuatavyo
- Utaweza kuchambua kwa undani post ambazo umezituma ili kujua zimefikia watu wangapi, wangapi wamevutiwa,wamezipenda, wamekoment katika post hizo (insights)
- Utaweza kutangaza post unazotaka na uweza kufanya matangazo mengine
- Unaweza post bidhaa yako na watu wakaiangalia/wakainunua kwa kuingia mtandaoni kupitia link na kuiona bidhaa hiyo (shopping post)
- Utaweza kuwa na batani ya “Contact” na aina ya kipengele cha bashara (category) ambayo unafanya
- Vile vile kwa kutuia mitandao kama Later.Com unaweza weka ratiba ya post zako na baadae zijipandishe zeyewe katika mtandao wa instagram (schedule posts)

Maana Ya Akaunti Ya ‘Creator’ Katika Mtandao Wa Instagram!
Hawa ni kundi la tatu la aina za akaunti katika mtandoa wa Instagram.. Hawa wapo kati ya Personal na Business na hi ni mahususi kwa wale ambao vioo vya jamii, wale wa youtube (yuotubers), washawishi (influencers) n.k
Ukiwa na akaunti ya aina hii unaweza kufanya yafuatayo
- Utaweza kuchambua kwa undani post ambazo umezituma ili kujua zimefikia watu wangapi, wangapi wamevutiwa,wamezipenda, wamekoment katika post hizo (insights) lakini hutaweza ku’shedule posts
- Vile vile unaweza kuficha batani ya ‘contact’ na aina ya kipengele cha biashara ila akaunti yako ionekane kama ni akaunti ya kawaida tuu

Ni Aina Ipi Ya Akaunti Inabidi Uwe Nayo?
Natumai kabisa hili swali sina mamlaka ya kulijibu kabisa sio? Sababu ni kwamba inategemea na wewe uko tayari kuanzia akaunti ya aina gani ambayo itakufaa kwa matumizi yako.
Kwa habari kama hizi za kiteknolojia na nyingine katika wigo wa sayansi usisite kutembelea mtandao wako pendwa wa TeknoKona kila siku ili kuhabarika
Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!
No Comment! Be the first one.