Kama wewe ni mmoja kati ya watumiaji wa vifaa vya Apple pengine unaweza ukawa unawaza mbona huwezi kushare mafaili mbali mbali kwa kutumia Bluetooth? Ndio jambo hilo haliwezekani kabisa. Apple hawaruhusu watumiaji wake ku share mafaili mbali mabali kwa kutumia njia hiyo iliyozoeleka na watu wengi.
Katika toleo la iOs 7, Apple walianzisha kipengele kipya katika simu yao kinanachoitwa AirDrop, ambacho kinaweza kuwa kama ni njia ya kuhamishia vitu kati ya iPhone, iPad na Mac. Katika makala hii teknokona itakujuza namna ambavyo unaweza ‘share’ mafaili kati ya vifaa hivyo vitatu vya Apple
Airdrop inapatikana katika matolea mapya ya iPhone na Mac. Matoleo hayo ni kama yafuatayo
- iPhone : iPhone 5, iPhone 5C, iPhone 5S, iPhone 6, iPhone 6 Plus
- iPad : iPad Mini, iPad Mini 2, iPad Mini 3 , iPad(4th generation), iPad Air, iPad Air 2
- iPod : iPod Touch(5th generation)
— Bila kusahau matoleo yote hapo juu lazima yawe yana endeshwa na iOs 7 au zaidi kama Programu endeshaji.
Kama una kifaa cha Apple ambacho kinakidhi maelezo ya hapo juu basi unaweza kuendelea
- Kwanza kabisa washa Airdrop katika kifaa chako ambo unataka kuhamisha mafaili. Utaweza fanya hivyo kwa kuingia katika ‘control center’ kama inavyoonyeshwa katika picha chini
- Bofya Airdrop ili kuweza kupatikana na watu, unaweza chagua watu katika simu (contact) tuu ndio wakuone au kila mtu
- Ukiwasha Airdrop, itawasha WiFi na Bluetooth, Katika Mac unaweza ipata Airdrop katika ‘Finder’
- Haya sasa twende katika kifaa ambacho tunakitumia picha sasa (Ngoja tutume picha)
- Ingia katika picha, bofya picha kuichagua na kisha bofya katika ki alama cha ku ‘share’ katika upande wa kushoto chini
Kama ulikua umewasha Airdrop, simu itaanza tafuta vifaa vilivyowasha Airdrop kama tuu bluetooth inavyofanyaga kazi. Kama hukuwasha Airdrop iwashe kwa kubofya juu yake.
Chagua kifaa cha Apple ammbacho unataka kutuma faili hilo kulingana na majibu yaliyokuja baada ya kutafuta vifaa hivyo.
Bofya ili kukubali kifaa cha kukitumia mafaili
Mpaka hapo umeweza kutuma mafaili katika ya vifaa vya Apple yaaani iPhone, iPad na Mac. Wengi wanasema simu za vifaa vya Apple ni vigumu sana kuvitumia kwani vina vipengele vingi vya kipekee. Inaweza ikawa ni kweli lakini bado ni kampuni kubwa sana katika masuala ya simu na inafanya vizuri kadri siku zinavyozidi kwensda.
No Comment! Be the first one.