Takribani miaka 24 iliyopita kampuni ya NCR na AT&T zilishilikiana kuanzisha teknolojia ya Wi-Fi, miaka mingi imepita, maboresho ya hapa na pale katika teknolojia hii yamefanyika. Pamoja na hayo yote bado teknolojia hii ya Wi-Fi imekuwa na changamoto nyingi kama vile muingiliano na huduma nyingine kama bluetooth, urahisi kwa wadukuzi kuutumia,na mwendokasi usioendana na teknolojia.
Kutokana na changamoto zilizojitokeza juu ya Wi-Fi Chama cha biashara kinachojulikana kama Wireless Gigabit Alliance kiliamua kukaa na kuja na aina nyingine ya mfumo wa mawasiliano mawasiliano ambayo inafanana na Wi-Fi, njia hii ambayo imepewa jina la Wi-Gig kimuundo na ufanyaji kazi wake ni kama ule ule wa Wi-Fi ila zipo tofauti kadhaa baina ya teknolojia hizi mbili. Ili tuielewe vizuri Wi-Gig basi basi nitafafanua tofauti zake kuu (nne) na mfumo wa zamani wa Wi-Fi.
1. Teknolojia ya Wi-Fi inafanyakazi kwa kurusha mawimbi katika masafa mafupi(low frequency) kama ilivyo kwa huduma nyingine nyingi na hili hupelekea kuwa na muingiliano ambao hupunguza ufanisi, kwa teknolojia ya Wi-Gig yenyewe inafanyakazi kwa kutumia mawimbi yanayo rushwa katika masafa marefu hadi GHz 60 katika masafa haya hakuna vifaa vingi hivyo hakuna muingiliano.
2. Ki-usalama mfumo wa Wi-Fi umekuwa ukikosolewa kutokana na ukweli kwamba ni rahisi sana kufanya udukuzi katika mfumo huu; Hili lina pande mbili; moja, mawimbi ya Wi-Fi husafiri umbali mrefu zaidi (hadi mita 90 sehemu ya wazi) hii inawapa nafasi zaidi wadukuzi kwa maana yakwamba haitaji kuwa ndani ya jengo lako(offisi yako) kukudukua ila hata akipaki gari lake karibu anaweza kuupata mtandao wako. Mbili, mtandao wa Wi-Fi hauna njia imara ya kuzilinda taarifa zilizomo katika mtandao, kwa ujuzi wa kawaida tu mtu akiwa ndani ya mtandao anaweza kuzipata taarifa hata ambazo hazimuhusu. Ukijumlisha haya mapungufu mawili unapata udhaifu mkubwa wa Wi-Fi kiusalama.
Wi-Gig kwa upande wake imebuniwa kuyakwepa mapungufu ya Wi-Fi kama ifuatavyo; moja, Wi-Gig inatumia mawimbi ya masafa marefu (high frequency) 60GHz, hii inamaanisha kwamba mawimbi yake hayawezi kusafiri umbali mrefu saana kama kwa Wi-Fi hii inafanya huu mfumo uwe mgumu kidogo kwa wadukuzi kuupata maana ita wahitaji kuwa ndani ya jengo ama ofisi husika. Mbili hata ukiwa ndani ya mtandao huu (Wi-Gig) bado hutaweza kuzipata data ambazo hazikumaanishwa kutumwa kwako, yaani katika mfumo huu kifurushi kikitoka katika ruta huwa encrypted na funguo ya kufungua kifurushi hiki hutumwa kwa kifaa kinachopokea kifurushi hicho maana yake yeyote atakae ingia kati hatoweza kufungua kabisa kifurushi hiki.
3. Wakati kwa kutumia Wi-Fi mwendokasi tunaweza kupata ni mpaka 100mbps hii inasababisha iwe ni vigumu kushusha vifurushi vikubwa kwa muda mfupi. Kwa kutumia teknolojia ya Wi-Gig tunaweza kufika speed mpaka 7Gbps, hii inaufanya huu mfumo wa Wi-Gig kuwa mfumo mahususi inapokuja swala la kusafirisha data nyingi kwa wakati mdogo.
4.Muda ambao pakiti ya data unatumia kusafiri kutoka kifaa kimoja hadi kingine ni mrefu zaidi kwa mfumo wa Wi-Fi kushinda ule wa Wi-Gig, hii ndiyo inayo changia Wi-Gig kuwa na mwendo kasi mkubwa zaidi ya Wi-Fi
Tayari makampuni mengi makubwa ya utengenezaji wa vifaa vinavyotumia mifumo hiiikama DELL yamekubali kutengeneza vifaa ambavyo viatumia mfumo wa Wi-Gig , pia na makampuni ya mitandao kama CISCO pia yameukubali mfumo huu.
Wireless Gigabit Alliance wanasema ya kwamba Wi-Gig haijaja kuiondoa Wi-Fi, ila imekuja kuziba mianya ambayo mfumo huu wa Wi-Fi haukuwa umejidhatiti. Mabaya ya Wi-Fi yatafichwa na Wi-Gig na hivyo kuleta mfumo bora zaidi.
Usisite kutuandikia kwa maoni ushauri ama maswali!
No Comment! Be the first one.