fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Apple IPhone simu Teknolojia

iPhone mpya huenda zikatoka Septemba 14

iPhone mpya huenda zikatoka Septemba 14
Spread the love

Mwezi wa kenda kwa Apple hufaaamika kuwa mahususi kwa ajili ya kutoa toleo jipya la iPhone inayofuata. Mwaka huu huenda tukaona bidhaa hizo mnamo Septemba 14.

Mwaka hadi mwaka  mwezi Septemba Apple huzindua toleo jipya la iPhone isipokuwa tu mwaka jana ambapo janga la virusi vya Korona lilisababishwa kusogezwa mbele kwa shughuli na zikazinduliwa mwezi Oktoba. Mwaka huu inaonekana Apple wamedhamiria kuendelea na mtindo wao uleule wa miaka yote hivyo tutegemee kuona toleo mbalimbali za iPhone 13 mnamo Septemba 14.

Simu janja ambazo zinatazamia siku ya Jumanne ya pili ya mwezi Speptemba ni iPhone 13, iPhone 13 Pro, iPhone 13 Pro Max na iPhone 13 Mini ambazo zote zinaaminika zitaweza kuagizwa kabla ya kuingia sokoni siku chache baada ya kuzinduliwa.

Septemba 14

Zinazoaminika kuwa iPhone 13 katika muonekano wa sura ya nyuma.

Ni lini zitaanza kununuliwa kabla ya kuingia sokoni?

Shughuli ya kuwa na uwezo wa kuagiza bidhaa kabla ya kuingia sokoni huwa ina faida zake hasa kwenye punguzo ukilinganisha na bei halisi ikishaanza kuuzwa rasmi. Kama uzinduzi wa iPhone zijazo kwa mwaka huu utafanyika Septemba 14 basi tutegemee kuwa na uwezo wa kuanza kuzinunua kuanzia Septemba 17.

Septemba 14

iPhone 13 (Bila Uhakika): Simu hizi huenda zikaingia sokoni rasmi mnamo Septemba 24.

Hiyo ndio habari ya iPhone mpya ambazo zinatazaniwa kutoka wiki chache zijazo. Tukusihi tuu kuendelea kutufuatilia kupitia mitandao yetu mbalimbali ya kijamii ili uhabarike.

Vyanzo: Gadgets 360, mitandao mbalimbali

SOMA PIA  ZIfahamu sifa zote za simu janja Xiaomi Mi 11

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania