fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Apple Saa Samsung Teknolojia

Mauzo ya saa janja yaongezeka vilivyo kwenye robo ya pili ya mwaka

Mauzo ya saa janja yaongezeka vilivyo kwenye robo ya pili ya mwaka
Spread the love

Mauzo ya saa janja yaendelea kufanya vizuri mara baada ya kuonekana kuongezeka katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka 2021 ambapo makampuni makubwa yaendelea kujitutumua.

Mahitaji ya saa janja bado yaonekana kuwa ni kiungo muhimu ambacho kinaingizia makampubi faida kubwa. Hii inachagizwa na ukuaji wa teknolojia ambapo saa hizi zinasaidia katika kufuatilia afya zetu kwa karibu, kuwa mbadala wa simu bila kusahau kutuonya muda ambao daima ni MALI.

Takwimu zinaonyesha hadi katika robo ya pili ya ya mwaka 2021 mauzo ya simu janja yameongezeka kwa 27% huku Apple wakijipatia zaidi ya $100 milioni kutokana na mauzo ya saa janja zao.

kwenye robo ya pili

Mauzo ya simu janja yaongezeka kwa 27% katika kipindi cha robo ya pili: Ingawa Apple imeendelea kuwa kinara lakini mauzo yake yameshuka kidogo kulinganisha na kipindi kama hiki mwaka uliopita.

Mauzo ya saa janja zaApple yameonekana kushuka kutokana ushindani kutoka kwa makampuni mengine kama Samsung na Garmin ambapo biashara yao ya saa janja imekuwa kwa 43% na 62% katika kipindi cha mwaka hadi mwaka. Galaxy Watch 3 na Watch Active 2 ni saa janja ambazo zimeonekana kuuzika zaidi ingawa hazijafikia umaarufu wa Apple Watch Series 6.

kwenye robo ya pili

Apple Watch Series 6 ndio imechagiza Apple kuongoza kwa 52% ya mauzo yote kwenye robo ya pili ya mwaka 2021 na ikionekana MArekani ndipo ilipouzika kwa wingi kulinganisha na maeneo mengine.

Masoko ya makubwa ya simu janja

Bara la Amerika Kaskazini ndio soko namba moja la simu janja, Uchina ipo nafasi ya pili kwa saa janja kuuzika huko. Mwaka uliopita India ilionekana kuchangia chini ya 2% ya mauzo lakini mwaka huu mambo yamekuwa tofauti kwa kuongezeka na kufikia 6% ndani ya kipindi cha mwaka mmoja tu hivyo kuifanya ndio soko la saa janja linalokuwa kwa haraka zaidi.

kwenye robo ya pili

Saa janja zilizouzika zaidi kwenye robo ya pili ya mwaka 2021.

Tangu mwaka huu uanze hadi mwezi Agosti mauzo ya simu janja yameongezeka kwa 47% na Huawei wameonekana kutofanya vizuri kama ambavyo takwimu zimeonyesha.

Vyanzo: Counterpoint, Engadget

SOMA PIA  Fahamu Teknolojia Ya Infinix NOTE 7!
Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comment

Comments

  1. […] za mauzo ya simu janja kwa mwezi Julai pekee huko Uchina zinaonyesha kwa makampuni makubwa kama Apple kuzidiwa nguvu na […]

  2. […] imesogea na teknolojia imekua pia; saa tulizokuwa tulizovaa miaka 10, 20, n.k iliyopita ni tofauti sana na hizi za leo ambazo zina mengi mbali ya […]

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania