Matumizi ya simu yameongezeka mara dufu hasa tangu ujio wa simu janja ambazo kila leo makampuni yanatoa simu zilizo bora kuliko zilizopita. Mwanamke mmoja anaweza akalipa faini kutokana na kuchati wakati alipokwenda sinema na mpenzi wake.
Wakati unapokuwa mahali na hasa kama upo na mwenza wako au kwenye kadamnasi kile unachokifanya kinaweza kisiwavutie wale walio karibu yako na matokeo yake ukawa unawakwaza.
Mwanamume mmoja katika jimbo la Texas, Marekani anadaiwa kumshhtaki mwanawake ambaye aliyekuwa amemlipia wakatazame sinema walipokuwa wanachumbiana lakini akaanza kutumia simu yake kutuma ujumbe kwa mtu mwingine.
Brandon, ambaye ndio mlalamikaji anadai kwamba dakika 15 baada yao kuanza kutazama filamu, mwanamke huyo alianza kutuma ujumbe kwa kutumia simu yake. MWanamke huyo alitumia simu angalau mara 10-20 katika kipindi cha dakika 15.
Soma pia: Mwanamke aachwa saa chache baada ya ndoa yake
Bw. Brandon alipoona kuwa uvumilivu umemshinda aaumuomba aende akatumie simu nje ya ukumbi wa sinema; mwanamke huyo aliondoka na kwenda zake kabisa na hakurejea.
Wengi wamekosoa kitendo cha mwanamke huyo cha kuchati wakati alipokuwa sinema na kwenda mbali kuwa mwanamke huyo anafaa hata kufungwa. Mlalamikaji anataka alipwe na mwanake huyo $17.31 ambacho kilikuwa ni kiingilio kwenye jumba la sinema. Wewe je, una maoni gani?
Chanzo: BBC