iPad Pro inasifa ya kuitwa moja ya kitu ambacho Steve Jobs alisema kamwe kampuni hiyo haitakuja kufanya…lakini mambo yanabadilika na sasa Apple wamegundua hakuna jinsi ni vizuri kukubali uhitaji wa mabadiliko. Apple wamekuja na iPad Pro ambayo kwa kiasi kikubwa imeiba mambo mengi kutoka kwa mpenzani wake, Microsoft, kwenye tableti zake za Surface.
iPad Pro kama vile ilivyo kwa Surface kutoka Microsoft ni vifaa ambayo ni zaidi ya tableti, kwa kifupi unaweza ziweka kati kati la tableti na laptop. Hii ni kwa sababu ni kubwa sana na pia zinakuja na chaguo la kutumia keyboard.
iPad Pro ina sifa gani?
iPad Pro ina ukubwa wa inchi 12.9, ni kubwa kweli kweli, hizi ni takribani sentimita 32.7. Na ni nyembamba kweli kweli ikiwa na upana wa mm 6.9 (takribani sentimita 0.69). Kioo chake kinakupa kiwango cha resolution cha 2732×2048, ni HD.
Pia inakuja na keyboard ambayo lazima ununue kivyake kwa gharama ya karibia laki 4. Ukilinganisha na keyboard kwa ajili ya tableti ya Surface kutoka Microsoft wengi wamesema keyboard ya iPad Pro sio nzuri sana, wakati ya Surface unaweza ukatumia kuandikia kwa urahisi zaidi hii inaitaji iwe mezani na inaitaji utulivu zaidi.
Kumbuka iPad aina alama maarufu ya ‘Arrow’, kimshale, hivyo utumiaji wa keyboard hii ni hasa kwa ajili ya kuandikia. Ila pia vifupisho (shortcuts) mbalimbali zinafanya kazi kama vile kwenye kompyuta. Ukibofya kwa pamoja Command na Tab utaweza kuangalia apps zote ulizofungua tayari. Command na C itakuwezesha kucopy data.
Penseli – Steve Jobs alikuwa anazichukia na kamwe alisema hazitakuja ila sasa zimekuja. Utumiaji wa penseli spesheli inayofahamika kama Stylus kwa ajili ya uchoraji n.k. Kama ushawahi kutumia simu za Samsung Note basi utakuwa ushawahi kukutana na kifimbo kidogo kinachokuja na simu hizo, basi hii Stylus ni kifaa kama hicho. Stylus itapatikana kwa takribani Tsh laki 2.Sifa zinginezo;
- Kwa upana wake utaweza kufungua apps mbili kwa wakati mmoja kwa wakati mmoja, zote zikionekana na wewe kuweza kuzitumia.
- Diski ujazo wa 32GB
No Comment! Be the first one.