fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
simu

iPhone 6s vs Samsung Galaxy S6: Nani Zaidi?

iPhone 6s vs Samsung Galaxy S6: Nani Zaidi?

Spread the love

Baada ya Apple kutambulisha rasmi simu mpya ya iPhone 6S swali la kujiuliza kwa wapenzi wengi wa simu za kisasa ni je kati ya iPhone 6S na Samsung Galaxy S6 ipi ni bora zaidi? Kampuni hizi zinategemea sana matoleo hayo mawili kwa kuwaletea faida zaidi mwaka huu.

Teknokona tutakuelezea kwa undani upate kufahamu ipi ni kali zaidi kwa kuzilinganisha kiundani. Kiukweli ushindani ni mkali sana na mwisho tungependa kusikia kutoka kwako pia kwa mtazamo wako wa ipi ni bora zaidi.

Simu ya Samsung Galaxy S6 na iPhome 6S

Simu ya Samsung Galaxy S6 na iPhome 6S

iPhone 6S vs Samsung Galaxy S6: Ukubwa na Uzito

Samsung Galaxy S6 ndiyo nyembamba zaidi ikiwa na kipimo cha milimita 6.8 wakati iPhone 6S ina upana wa milimita 7.1.

iPhone 6S vs Samsung Galaxy S6: Kioo (Display)

Kwenye kioo nguvu kubwa kwa iPhone 6S ni utumiaji wa teknolojia mpya ya ‘Force Touch’, kupitia teknolojia hii simu itaweza kutambua ni kwa kiasi gani unatumia nguvu kuigusa na hivyo apps zitaweza kukupa matokeo tofauti kulingana na wewe utakavyogusa app hiyo. Huawei ndio walikuwa wa kwanza kutumia teknolojia hii katika simu yao ya Mate S na sasa Apple wameanza itumia pia. Apple wamitumia kwenye saa zao za Apple Watch na baadhi ya MacBooks mpya.

Utumiaji wa Force Touch

Utumiaji wa Force Touch

 

SOMA PIA  Urusi yadai kampuni kubwa za kiteknolojia kufungua ofisi zao nchini ifikapo 2022

Ukitoa utofauti huo sehemu nyingine utofauti wa ukubwa wa display zake, Samsung Galaxy S6 ni kubwa zaidi ikiwa na kioo cha inchi 5.1 wakati iPhone 6S ina kioo cha inchi 4.7. Pia kwenye ‘resolution’ yaani kiwango cha ubora wa muonekano (HD), Galaxy S6 ipo juu zaidi ikiwa na resolution ya 1440×2560 ukilinganisha na 750×1334 cha iPhone 6S. Ukilinganisha ukubwa wa kioo cha ujazo wa pixels kwa kila inchi moja ya kioo hicho Galaxy S6 ina pixels 577 kwa kila inchi moja wakati iPhone 6S ina pixels 326. Viwango vya pixela vimekuwa vikubwa sana katika simu janja siku hizi ja wengi wanaona limekuwa sio jambo la kuangalia sana kwani viwango vyote katika simu hizi ni vya juu na vinalizisha.

 

iPhone 6S vs Samsung Galaxy S6: Kamera

iPhone 6S ina kamera ya nyuma ya MP 12, ni maboresho ukilinganisha kiwango cha MP 8 kwa toleo lililopita ila Galaxy S6 ndio ipo juu kwa kiwango cha MP 16. Ubora wa picha pia unategemea mambo mengine mengi zaidi ya viwango vya sensor za kamera na makampuni yote mawili yana sifa kubwa katika eneo la kamera zenye picha bora zaidi.

SOMA PIA  Baada ya KitKat Google Waja na Android L

Kwenye selfi yaani kamera za nyuma simu zote mbili zina kamera ya MP 5.

 

iPhone 6S vs Samsung Galaxy S6: Ujazo wa Diski Uhifadhi, RAM na Prosesa

Kwenye suala la memori kadi yaani SD Card siku hizi simu za Galaxy haziji na eneo hilo tena na sifa hii dhidi ya simu za iPhone imepoteza. Samsung Galaxy S6 inakuja na matoleo ya GB 32, 64, na 128, wakati iPhone 6S inakuja na matoleo ya GB 16, 64 na 128. Wengi wanachukizwa na uamuzi wa muda mrefu wa Apple kuanza na ujazo wa GB 16, kwani kwa wengi siku GB 16 ni haitoshi kabisa wakati gharama ya Apple kutumia ujazo wa GB 32 hautaongeza ghara,a yeyote kubwa kwa simu hizo. Labda hii ndio mara ya mwisho..

Samsung Galaxy S6 imekuwa moja kati ya simu bora na ya kiubunifu zaidi kutoka kampuni ya Samsung.

Samsung Galaxy S6 imekuwa moja kati ya simu bora na ya kiubunifu zaidi kutoka kampuni ya Samsung.

Kwenye RAM Apple huwa wasiri kusema rasmi kwenye utambulisho ila tayari mfanyakazi mmoja wa kampuni hiyo amemwaga siri kupitia mtandao wa Reddit ya kwamba simu hizo zinakuja na GB 2 za RAM, Galaxy S6 ina RAM ya GB 3.

SOMA PIA  Ifahamu vyema simu janja Samsung Galaxy A52s 5G

Prosesa kulinganisha ni vigumu pia kwani zote zinatumia teknolojia tofauti kabisa. Tunachofahamu kwa sasa ni kwamba prosesa ya iPhome 6S ni bora kwa ukasi wa zaidi ya mbili ukilinganisha na ile iliyotumika kwenye toleo la iPhone iliyopita. Samsung Galaxy S6 inatumia prosesa ya kisasa tuu – Octa Prosesa yenye chipu moja ya Quad-core yenye ubora wa Ghz 1 na nyingine Ghz 2.1

iPhone 6S vs Samsung Galaxy S6: Bei

Bei ya iPhone 6S

GB 16 – Dola 649 za Kimarekani ( Milioni 1.4 za Kitanzania) ,

GB 64 – Dola 749 za Kimarekani ( Milioni 1.6 za Kitanzania) ,

GB 124 – Dola 849 za Kimarekani ( Milioni 1.8 za Kitanzania) ,

Samsung Galaxy S6

GB 32 – Dola 684 za Kimarekani ( Milioni 1.5 za Kitanzania) ,

GB 64 – Dola 786 za Kimarekani ( Milioni 1.7 za Kitanzania) ,

GB 124 – Dola 864 za Kimarekani ( Milioni 1.87 za Kitanzania) ,

 

Huo ndio mlinganisho wa simu hizi za viwango vya juu kwa sasa, tuambie mshindi ni yupi lwa mtazamo wako? Ukiwa na uwezo wa kununua moja wapo utanunua ipi na kwa nini?

 

Comrade Mokiwa

Mbunifu na mpenda teknolojia.

Muanzilishi wa Teknokona, TechMsaada na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Comments

  1. Samsung s6 is the best than iPhone 6

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania