Katika ulimwengu wa simu janja sasa, kuibiwa au kupoteza kifaa chako sasa ni jambo la kawaida kutokana na mihangaiko mbalimbali ya maisha. Baadhi ya watu, huthubutu hata kuamini kuwa, kupoteza simu zao si kitu, bali data kama picha, maongezi ya ujumbe wa simu na WhatsApp, au hata majina na namba za wapendwa wao kupotea kabisa.
Kupoteza simu janja yenye data muhimu kama izo hapo juu, huenda kukakwamisha na hata kuhatarisha faragha za watu. Watu wengi huchanganyikiwa, kushindwa kujua cha kufanya na kuhuzunika kwa masiku.’
Lakini, si kitu tena kwa watumiaji wa iPhone, iPod Touch na iPad. Kupitia iCloud kwenye kompyuta au kifaa kingine chochote chenye internet, unaweza kupata eneo simu yako ilipo, kufuta kila kilichopo katika simu yako hata kama ipo mbali au kuifunga simu yako, na mwizi/ mtu mwingine asiweze kuifungua kwa namna yeyote ile. Ndio, inawezekana.
Fuata hatua zifuatazo, ili kuweza kuilinda iPhone/iPad/iPod yako dhidi ya wizi, au upotevu wa data.
1. Hakikisha umefungua akaunti yako ya iCloud, na umewasha kitufe cha ‘Find My iPhone/iPod au iPad katika kifaa chako. Hapa unaiunganisha simu yako na mtandao kabla hujaipoteza. Ni muhimu. Nenda Setting > iCloud > Find My iPhone. Hakikisha iko ON.
Kama uliwasha Find My iPhone katika simu yako iliyopotea, unaweza ukaitumia Find My iPhone hiyo kupata simu yako au kuchukua hatua nyingine ambazo zinaweza zikakusaidia kulinda data zako katika simu, iPod au iPad yako.
a. Fungua mtandao wa icloud.com/find katika kompyuta yako. Unaweza pia kutumia App ya Find My iPhone katika simu nyingine, iPod Touch au iPad.
b. Ingiza akaunti yako na neno siri ulotumia wakati wa kusajili kifaa chako katika iCloud. Ingia, na utapelekwa kwenye ukurasa wako wa iCloud ambapo unaweza kuanza kufanya hatua za kuipata au kulinda data zako. Unaweza kufanya yafuatayo
c. Fungua ‘Find my iPhone’ na chagua kifaa chako katika orodha ya vifaa utakavyokua umesajili. Utaletewa Ramani inayokuonyesha kifaa kilipo, na kama kipo karibu utaweza kukipigisha sauti ili kukusaidia wewe au mtu aliye karibu nacho kukisikia.
d.Unaweza ukafunga kifaa chako kwa kutumia neno siri maalum, na kutuma ujumbe maalum kwenye kifaa chako, utakaojishikiza katika kioo cha simu yako, kama vile namba zako za simu na ujumbe wa kuomba kurudishiwa kifaa chako. Bonyeza ‘Turn On Lost Mode’ na utakua umedhibiti mtu yeyote kuifungua simu yako kwa namna yeyote.
e. Futa Kila kitu katika simu, iPad au iPod Touch yako. Pia ili kulinda mtu yeyote asione data zako katika kifaa chako ulichopoteza, unaweza ukafuta kila kilichomo hata ukiwa mbali nacho. Cha Msingi cha kujua apa ni kwamba, ukifuta kila kitu, hutaweza kuipata tena simu yako, hata kama ulijisajili katika ‘Find My iPhone’. Ukifuta kila kitu, unafuta hadi mipangilio yote ya kufunga simu yako uliyoiweka, na utamwezesha mtu mwingine kutumia simu yako bila matatizo.
VIPI KAMA KIFAA CHAKO KIMEZIMWA AU DATA ZA INTERNET ZIMEZIMWA?
Kama ikitokea hivi, bado unaweza ukafunga, ukafuta kila kitu, lakini mabadiliko haya yatafanyika punde tu kifaa hiki kitakapowashwa au kutumiwa katika Wi-Fi au data za internet.
VIPI KAMA NITAPATA KIFAA CHANGU?
Unaweza kuzima kwa kuingiza neno siri ulilochagua wakati wa kuwasha Find My iPhone. Utaingiza neno siri hilo katika simu yako au katika mtandao wa iCloud.
VIPI KAMA HUKUWASHA ‘FIND MY iPHONE’ KATIKA KIFAA CHAKO KABLA HUJAPOTEZA?
Katika hili, unashauriwa kufanya yafuatayo:
1. Badilisha neno siri la accouti yako ya iTunes na iCloud. Kwa kufanya hivi, utazuia shughuli zote zinazohusisha iTune na iCloud katika kifaa chako ulichopoteza.
2. Badilisha neno siri ya akaunti nyingine katika mitandao, mfano Facebook, Twitter, Instagram, Gmail au Yahoo. Hii ni ili kuweza Usalama wa akauti zako na faragha katika mitandao yako.
3. Ripoti katika mamlaka husika juu ya upotevu wa kifaa chako. Mamlaka wanaweza wakahitaji Serial namba za kifaa chako ambzo unaweza kuzipata katika kasha la simu iyo.
Find My iPhone ndio huduma pekee itakayowezesha kutafuta, kufuta au kulinda data za kifaa chako ulichopoteza. Hivyo, kama mtumiaji wa vifaa vya Apple, unashauriwa kujisajili na iCloud na kuwasha huduma ya Find My iPhone kwani Hakuna namna nyingine yeyote utakayoweza kutafuta, kuzima, kuifunga au kulinda data za kifaa ulichopoteza
No Comment! Be the first one.