iPhone ni simu janja ambazo zina umaarufu mkubwa sana duniani. Ni moja ya kampuni ambayo imeuza kopi nyingi za simu janja, mpaka sasa kampuni umeuza kopi zaidi ya bilioni moja kwa wateja wake.
Simu kama simu zinapata umaarufu wake sana kwa kuwa na vipengele ambavyo kwa namna moja au nyingine vitateka akili ya watumiaji. Sio siri kwamba vitu hivyo ndivyo huwa vinafanya watu wazikimbilie simu hizo na kuzinunua

Kampuni ya Apple inasemekana kuwa ina mpango wa kuchana na uwezo wa kutambua alama za vidole maarufu kama ‘Touch ID’ na kwenda katika ‘ 3D Face Scanning’ katika simu zake za iPhone
Face Scanning ni teknolojia ambazo inatumika katika kutambua sura ya mtu husika. Fikiria kwa kina kama teknolojia hii ikija katika simu itakuwa na mapunduzi ya aina yake

Utambuzi wa alama za vidole ni teknolojia ambayo ni maarufu sana kwa sasa na imeshazoeleka kwa watu wengi pia simu nyingi sana zinakuja na teknolojia hiyo.
Apple wanataka kuleta kitu ambacho kitakuwa ni cha kipekee katika simu zake, ripoti zimesema kuwa pengine Teknolojia hii inaweza ikaja katika toleo la iPhone 8.
Touch ID Kulinganisha Na 3D Face Scanning
Kuna mengi ya kutofautisha katika teknolojia hizi mbili. Kwa mfano katika ‘Touch ID’ kwenye simu za iPhone ni vigumu sana kutoa loki kama kidole chake kitakuwa na uchafu uchafu au maji maji. Yaani ni hizi alama za vidole hazitatmbulika katika iPhone kama kidole kitakuwa katika hali hiyo.

Uzuri ni kwamba teknolojia ya ‘3D Face Scanning’ ni bora zaidi ukilinganisha na ya ‘Finger Print’ hivyo basi mtumiajia wa iPhone anaweza akawa na usalama na ulinzi wa kutosha zaidi kama akitumia Teknolojia hii. Vile vile Teknolojia hii ni vigumu sana kufeli katika utumikaji wake ukilinganisha na ile ya alama za vidole.
Je iPhone 8 Itakuja Na 3D Face Scanning?
Bado ni swala kubwa ambalo mpaka sasa halina majibu kwani kampuni ya Apple pekee ndio inayojua hili. Tusubiri kutoka kwao pengine ndio watatufungua zaidi na kujua mengi kuhusiana na teknolojia hii.