fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Apple apps iOS 15 Teknolojia

iOS 15: Tegemea kuona ukiulizwa kama unataka kuona matangazo yanayokulenga

iOS 15: Tegemea kuona ukiulizwa kama unataka kuona matangazo yanayokulenga
Spread the love

Katika kitu ambacho ambacho kinawakera watu wengi duniani kote kwenye ulimwengu wa kidijitali ni matangazo ambayo yanajitokeza tuu bila mpangilio wowote ule.

Kiujumla matangazo kwenye vifaa vyetu vya kiganjani yamekuwa yakilamikiwa kwa miaka mingi tuu na hatimae Apple wanajipanga kufurahisha watu kwenye iOS 15. Apple imewalazimu kuwa wapole na kufuata maagizo ya wenye mamlaka mbali ya kulinda taarifa za wateja wao lakini suala la matangazo kutokea ni lazima liwe ni la hiari na si lazima.

SOMA PIA  Waanzilishi wa Instagram waacha kazi

Kwa mujibu wa Apple ambao wanatarajia kutoa iOS 15 wanasema toleo hilo la programu endeshi litakuwa linaomba watumiaji wake waruhusu uwezo wa kuapata matangazo “Yanayolenga mhusika mwenyewe”. Msingi wa hili unatokea vile ambavyo tunatumia simu janja zetu (iPhone) kuanzia programu tumishi tunazopakua mpaka yale tunayoperuzi mtandaoni.

iOS 15

Awali Apple ilikuwainaleta tuu matangazo kulingana na yale ambayo tunapendelea kupakua, kuperuzi kwenye rununu lakini mambo kuwa tofauti kwenye iOS 15 hivyo mtu kuwa na uhuru wa kupenda kuyaona au la!.

Apple pia imewaagiza watengezaji wa programu tumishi kutumika kwenye iOS kuacha kukusanya taarifa za wateja wao bila ridhaa ya mhusika ambapo baadae wanatumia taarifa hizo kupeleka matangazo kwenye rununu kulingana na kile ambacho inaonekana mtu anakipenda.

SOMA PIA  Mradi mkubwa kuliko yote duniani wa nishati ya Jua

Kwa upande mwingine matangazo si mabaya

Kutokea kwa matangazo kwenye rununu kiujumla yanatujulisha kuhusu kitu fulani ambacho ni kizuri kitafaa kwenye matumizi ya simu janja zetu hivyo kufanya kukusogeza karibu na kile ambacho ulikuwa ukikitafuta. Katika kuruhusu au kuzuia matangazo Apple wanaweka kipengele hicho ndani ya mpangilio (settings) hivyo kuwa rahisi kufanya mabadiliko kila utakapohitaji.

SOMA PIA  Clickfarms: Wauza Likes, Shares, na Comments wakamatwa nchini Thailand

Je, unafahamu ni lini iOS 15 itatoka? Kaa nasi na tutakufahamisha. Kumbuka kufuatilia TeknoKona ili uweze kuhabarika halikadhalika kuelimika kuhusu teknolojia.

Vyanzo: The Verge, mitandao mbalimbali

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania